MOJA kwa moja kutoka kwenye mdomo wa mhusika, yametoka maneno haya: "Nimemsamehe lakini nimeshamsahau." Haya ndiyo yaliyokuwa majibu ya Goldie kwa Big Brother baada ya kuulizwa kuhusu mahusiano yake na Prezzo.
Hakuna aliyedhani kwamba itafika siku Goldie atafikiria kuachana na Prezzo lakini jana ilionekana kwamba siku ya hiyo imewadia. Kila mwanamke ana ukomo wake wa kupenda na inaonekana sasa Goldie hatimaye amefikia ukomo wake. "Hakuna sababu ya kumfikiria yeye (Prezzo)," alisema kimwana huyo Mnigeria.
Inaonyesha ilikuwa inamchefua tabia ya mwanaume wake kumkumbusha vitu alivyomfanyia na kumnunulia mjengoni humo kila inapotokea wamekorofishana. "Kama inapotokea siku hauna furaha unaanza kunihesabia mara ngapi umeninunulia pafyumu, sasa kwanini ulinunua?" alisema Goldie.
Goldie akiwa na Prezzo ndani ya Jumba la BBA |
Kimwana huyo muimbaji pia hakuacha kumchana Prezzo kwa tabia yake ya kuwapa majina mabaya watu akiwemo yeye. "Hapana sikubaliani na hilo. Kwangu mimi sio sahihi."
Mapema siku hiyo, Goldie alisikika akiimba wimbo unaohusua kuachana na mpenzi.
Bila ya shaka usemi kwamba "mwanamke akichoka, amechoka" ni wa kweli.
No comments:
Post a Comment