Friday, June 29, 2012

BALOTELLI, PIRLO WAMTISHA FABREGAS

Kiungo wa timu ya taifa ya Hispania, Cesc Fabregas, akizungumza na vyombo vya habari pembeni ya mchezaji mwenzake Sergio Ramos leo Juni 29, 2012 mjini Kiev, Ukraine kuelekea mechi yao ya fainali ya UEFA Euro 2012 dhidi ya Italia.

KIUNGO wa timu ya taifa ya Hispania, Cesc Fabregas, anaamini kwamba Mario Balotelli na Andrea Pirlo ndio watu wa kuwadhibiti katika timu ya taifa ya Italia.

Nyota huyo wa Barcelona na wachezaji wenzake wa kikosi cha Hispania wanajiandaa na mechi ya fainali ya Euro2012 dhidi ya Italia itakayopigwa mjini Kiev Jumapili na ameonya kwamba nyota wa Juventus, Pirlo na mfungaji wa magoli mawili ya jana usiku Balotelli ndio watu wa hatari katika mechi hiyo ya kuamua bingwa.

"Tutalazimika kuwasimamisha washambuliaji wa Italia na Pirlo pia," Fabregas amesema leo katika mkutano na wana habari.

"Balotelli ni mchezaji mzuri na amethibitisha jana. Amefunga magoli mawili makali katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.

"Mabao yale yanasema kila kitu. Nimependa sana namna alivyocheza. Atakuwa tishio, kama Antonio Cassano au mchezaji mwingine yeyote."

No comments:

Post a Comment