Wednesday, June 27, 2012

FABREGAS KUANZIA BENCHI LEO, NEGREDO NDANI

Fabregas (kulia) akiwa na Sergio Busquets

DONETSK, Ukraine
MSHAMBULIAJI Alvaro Negredo amejumuishwa isivyotarajiwa katika kikosi cha Hispania kitakachoanza katika mechi itakayoanza dakika 45 zijazo ya nusu fainali ya Euro 2012 dhidi ya Ureno huku kocha Vicente Del Bosque akimuacha nje kiungo Cesc Fabregas.

Ureno imelazimika kufanyia mabadiliko kwa mara ya kwanza kikosi chao cha kwanza katika fainali za mwaka huu kutokana na mshambuliaji Helder Postiga kuwa na majeruhi wa paja na, kama ilivyotarajiwa, Hugo Almeida amechukua nafasi hiyo katika safu ya washambuliaji watatu pamoja na Nani na Cristiano Ronaldo.

Kitendo hicho cha Del Bosque kinamaanisha kwamba Hispania itakuwa na mshambuliaji anayefahamika baada ya kuwafunga Ufaransa 2-0 katika mechi yao ya robo fainali kujaza wachezaji sita katika kiungo lakini hakuna nafasi kwa Fernando Torres ambaye ameanzia benchi pamoja na mshambuliaji mwnzake Fernando Llorente.

Mshambuliaji wa Sevilla, Negredo, ambaye alidhaniwa kwamba kuwa chaguo la nyuma ya nyota hao wawili, amefunga magoli sita katika mechi 11 alizoichezea timu ya taifa ya Hispania lakini amecheza mara moja tu hadi sasa katika michuano ya sasa - akiwa ameingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 89 dhidi ya Croatia.

Vikosi vitakavyoanza leo baadaye:

Ureno: 12-Rui Patricio; 21-Joao Pereira, 2-Bruno Alves, 3-Pepe, 5-Fabio Coentrao; 16-Raul Meireles, 4-Miguel Veloso, 8-Joao Moutinho; 17-Nani, 9-Hugo Almeida, 7-Cristiano Ronaldo

Hispania: 1-Iker Casillas; 17-Alvaro Arbeloa, 15-Sergio Ramos, 3-Gerard Pique, 18-Jordi Alba; 16-Sergio Busquets, 14-Xabi Alonso; 8-Xavi, 6-Andres Iniesta, 21-David Silva; 11-Alvaro Negredo

Refa: Cuneyt Cakir (Uturuki)

No comments:

Post a Comment