Daniel Sturridge |
MCHEZAJI mpya aliyesajiliwa na Liverpool, Danny Sturridge amesema anajiandaa kucheza kama winga.
Kulikuwa na uvumi kwamba uhamisho wake wa kutoka Chelsea umekwama baada ya Sturridge kutaka achezeshwe kama mshambuliaji wa kati.
Aliiambia tovuti ya liverpoolfc.com: "Najiona mimi kama mshambuliaji. Nadhani nacheza vyema pale kwa sababu ya staili yangu ya uchezaji, naamini, ni bora kwa mshambuliaji wa kati. lakini nimekuwa nikicheza katika wingi na nimejifunza mengi katika kufanya hivyo. Siwezi kukataa kucheza pembeni na sijawahi kuomba nichezeshwe kati, pia.
"Kwangu, mahala popote kocha atakapotaka nicheze nitacheza kwa bidii zote kwa ajili ya klabu na mashabiki. Nitajaribu kuwafanya mashabiki watabasamu na kujaribu kuleta mafanikio katika klabu - itakuwa poa sana.
"Mimi nina kasi, napenda 'kuwapunguza' mabeki, kujaribu na kuwapikia nafasi wachezaji wenzangu, napenda soka la kwenda mbele, napenda kushuti na kupasia. Ni kujaribu na kusaidia timu ishinde. Kasi yangu itawasaidia wachezaji wenzangu kunifanya nifunge, lakini muhimu zaidi ni kufanya kazi kwa ajili ya timu na kuwasaidia wachezaji wenzangu kushinda mechi. Hicho ndicho muhimu kuliko chochote kingine, haijalishi kuhusu mimi binafsi. Ni kuhusu timu na kushinda mechi."
No comments:
Post a Comment