Obafemi Martins |
MSHAMBULIAJI wa Levante, Obafemi Martins ameunga undugu na familia ya mshambuliaji wa Manchester City, Mario Balotelli.
Kwa mujibu wa jarida la ‘Diva e Donna’ la nchini Italia, Abigail Barwuah – dada wa damu wa Balotelli – ni mjamzito.
Baba wa mtoto mtarajiwa anasemekana kuwa ni Obafemi, mshambuliaji mwenye umri wa miaka 28, ambaye amewahi kuchezea klabu za Inter Milan, Newcastle United, Vfl Wolfsburg, Rubin Kazan, Birmingham City na sasa Levante.
Jarida hilo limemnukuu dada huyo akisema: "Mtoto ameanza kujitingisha tumboni. Hii ni Krismasi 'spesho' sana kwangu."
Mwezi uliopita rafiki wa kike wa Balotelli, Raffaella Fico alijifungua mtoto wa kike waliyemuita Pia, ingawa mshambuliaji huyo wa Manchester City bado amesisitiza anataka vipimo vya DNA kabla ya kumtambua rasmi kama mwanae.
No comments:
Post a Comment