Tuesday, January 8, 2013

KWANINI MESSI NA RONALDO HAWAKUPIGIANA KURA?

Ronaldo, Iniesta na Messi wakihudhuria mkutano wa waandishi wa habari wa nyota watatu walioingia fainali ya kuwania tuzo ya FIFA Ballon d'Or  kwenye Ukumbi wa Congress House mjini Zurich, Uswisi jana  Januari 7, 2013

NAMNA ya kujipanga katika kukaa ukumbini wakati wa tuzo ilizingatia herufi zao hivyo Iniesta akajikuta akikaa katikati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Lakini hakuna kati yao wapinzani hao wakubwa aliyempigia kura mwenzake. "Kwanini?" unaweza kujiuliza...  majibu ni haya hapa...

Messi alidai kwamba wazo lake lilikuwa ni kuwapigia kura mchezaji mwenzake wa Barcelona na ndiyo maana akawachagua Xavi na Iniesta. Chaguo lake la tatu, lilikuwa mchezaji mwenzake wa timu ya taifa, Aguero. Hata hivyo... "Ingekuwa ni ujinga kutomfikiria Cristiano kama mmoja wachezaji bora. Nilifikiria tu kwamba hawa ndiyo wachezaji ninaopaswa kuwapigia kura," alisema Messi.

Cristiano Ronaldo alikuwa na sababu nzuri zaidi. Licha ya kuwa ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno hakuweza kupiga kura. Alikuwa majeruhi. "Niliumia wakati nikiwa na timu ya taifa hivyo nikarudishwa nyumbani. Sikupiga kura," alifafanua.


Kura za kuamua mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or ya Mwanasoka bora wa Dunia hupigwa na makundi matatu: makocha wa timu za taifa, manahodha wa timu za taifa na wawakilishi wa wanahabari kutoka kote duniani.

No comments:

Post a Comment