Tuesday, January 8, 2013

BARCA YAUFIKIA UBINGWA WA REAL MADRID WA BILA KUFUNGWA LA LIGA MWAKA 1931/32


Wachezaji wa Barcelona wakishangilia

KWA kupata pointi 52 katika ya 54 walizokuwa wakiziwania katika La Liga msimu huu, Barcelona tayari imeifikia rekodi yao binafsi ya pointi 52 katika nusu msimu.

Barca wana nafasi katika mechi yao ya wikiendi dhidi ya Malaga ya kuivuka rekodi hiyo waliyoiweka miaka miwili iliyopita katika msimu wa 2010/11, wakati walipopata pointi 52 kati ya 57 walizowania katika nusu ya kwanza ya msimu, ambapo walipoteza mechi moja na kutoka sare moja.

Kama watashinda dhidi ya Malaga, Barcelona watafikisha pointi 55 na bado watakuwa na mechi moja mkononi ili kukamilisha nusu ya kwanza ya msimu.

Msimu huu, mabingwa hao wa nusu msimu hawajafungwa mechi hata moja na wametoka sare moja tu katika mechi 18 walizocheza kufikia sasa. Sare pekee walitoka dhidi ya Real Madrid. Barcelona wanaongoza ligi kwa pointi za aina yake na kama wataendelea hivyo, wanaweza kuipiku rekodi ya pointi 100 iliyowekwa na Real Madrid msimu uliopita.

Changamoto nyingine kwa Barcelona ni kumaliza msimu bila ya kufungwa, jambo ambalo lilifanywa na timu mbili tu za Athletic Bilbao msimu wa 1929/30 na Real Madrid msimu wa 1931/32.

Hata hivyo, kipindi hicho, ligi ilikuwa na mechi 18 tu, idadi sawa na mechi ambazo tayari zimechezwa La Liga hivi sasa.

No comments:

Post a Comment