Thursday, December 27, 2012

RONALDO ANASTAHILI TUZO BALLON D'OR - FIGO


GWIJI wa Real Madrid, Luis Figo anaamini kwamba Cristiano Ronaldo anastahili tuzo ya Ballon d'Or.

Figo alisema mafanikio ya Ronaldo kwa mwaka huu yanapaswa kumshuhudia akitwaa tuzo hiyo adhimu.

"Nadhani Cristiano ana vigezo vyote vya kushinda Ballon d'Or, daima anakuwa katika nafasi ya mbele kuelekea kushinda tuzo yoyote, alikuwa na kampeni nzuri katika ligi, Ligi ya Mabingwa Ulaya na daima hufunga magoli.

"Lakini, kwa inavyofahamika, mataji binafsi yanatokana na mitazamo binafsi ya watu wengi na daima ni vigumu kujua nani atashinda," alisema balozi huyo wa klabu ya Inter Milan.

No comments:

Post a Comment