Pepe akifurahi baada ya kushinda tuzo ya 'Person of the Year |
BEKI wa Real Madrid, Pepe ameshinda tuzo ya 'Person of the Year' inayoandaliwa na gazeti la Record la nchini Ureno.
Washindi wa siku za nyuma wa tuzo hiyo ni pamoja na mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na kocha José Mourinho.
Pepe alisema: “Nina furaha sana kushinda tuzo hii na nafarijika kwa sapoti ninayopata kutoka kwa watu ambao wananiamini. Ni heshima kubwa na napeleka shukrani kwa wachezaji wenzangu kwa sababu bila ya wao nisingeweza kushinda tuzo hii. Nina furaha sana na najisikia kupagawa kupokea tuzo hii."
Ronaldo na Fabio Coentrão walihudhuria sherehe za tuzo hiyo na wakampongeza Pepe.
No comments:
Post a Comment