Friday, December 28, 2012

RADAMEL FALCAO ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWAKA 2012...NI TUZO INAYOTOLEWA KILA MWAKA NA GLOBE SOCCER... AWAPIKU LIONEL MESSI NA CRISTIANO RONALDO BAADA YA KUWAPIGA CHELSEA HAT-TRICK NA KUIPA ATLETICO MADRID TAJI LA SUPER CUP LA ULAYA... PIA ALIISAIDIA KLABU YAKE ATLETICO MADRID KUTWAA UBINGWA WA LIGI YA EUROPA MWAKA 2012

Radamel Falcao
Natishaaaaaa....! Radamel Falcao akishangilia baada ya kutupia bao.
DUBAI, Falme za Kiarabu
Straika wa klabu ya Atlético de Madrid ya Hispania, Radamel Falcao atakabidhiwa zawadi yake baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka 2012 ya Globe Soccer, ambayo hafla yake inafanyika jijini Dubai leo Desemba 28 na kesho (Desemba 29).

Falcao anayejulikana pia kwa jina la utani la 'The Tiger', alikuwa katika kiwango cha juu mwaka 2012. Alifunga jumla ya magoli 49 na pia kuisaidia Atlético kutwaa mataji mawili. Mcolombia huyu alithibitisha umuhimu wake katika kila michuano baada ya kufunga magoli mawili katika fainali ya Ligi ya Europa na kuipa ubingwa Atletico na pia akapiga 'hat-trick' katika fainali ya kuwania taji la Super Cup la Ulaya dhidi ya Chelsea na kuipa ubingwa klabu yake kutokana na ushindi wa 4-1.

Kwa sababu ya tuzo yake na pia kulazimika kuhudhuria hafla hiyo jijini Dubai, Falcao atachelewa kuanza mazoezi na wenzake klabuni Atlético.

Atlético imepanga kuanza kujifua kesho Jumamosi (Desemba 29) baada ya mapumziko ya Krismasi, lakini Mcolombia huyo anatarajiwa kuungana na kocha wake Simeone na  wachezaji wengine keshokutwa Jumapili (Desemba 30).

Mbali na Falcao, Atlético imeteuliwa pamoja na Chelsea, BATE Borisov na Juventus kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka. Miguel Ángel Gil Marín wa Atlético pia yuko jijini Dubai baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mkurugenzi Bora wa Klabu.

No comments:

Post a Comment