Friday, December 28, 2012

MESSI AONGOZA WALIOZIFUNGIA TIMU ZAO ZA TAIFA MAGOLI MENGI MWAKA 2012... ANAFUATIWA NA ZLATAN IBRAHIMOVICH

Lionel Messi

MWAKA 2012, Messi hatimaye amekuwa nyota wa mabao wa Argentina baada ya kushindwa kwa miaka mingi kuhamishia kwenye timu yake ya taifa makali yake ambayo amekuwa akiyaonyesha Barcelona.

Maswali kuhusu tofauti ya kiwango cha Messi awapo Barcelona na anapoichezea timu ya taifa ya Argentina yanaonekana kupata majibu baada ya kuwasili kwa kocha Alejandro Sabella kwenye benchi la ufundi la Argentina.

Messi ndiye aliyeibuka kuwa mfungaji magoli mengi zaidi duniani ndani ya mwaka mmoja 2012 baada ya kufunga mabao 91, huku mabao 12 akiifungia timu ya taifa ya Argentina.

Huku akiwa amempita kwa goli moja Zlatan Ibrahimovic (ambaye ameifungia timu yake ya taifa ya Sweden magoli 11 mwaka 2012), Messi ametangazwa kuwa mchezaji aliyeifungia timu yake ya taifa mabao mengi zaidi katika mwaka 2012, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwake kufanya hivyo. Kufikia sasa, takwimu za mabao za nyota huyo wa Barcelona kwenye timu yake ya taifa ya Argentina zimekuwa ni ndogo kulinganisha na zile za klabu.

Mwaka wake bora katika katika ngazi ya taifa ulikuwa 2007, ambapo alifunga magoli sita kwa  Argentina, yakiwamo mawili yake ya kwanza katika mechi moja, ambayo ilikuwa ni ya kirafiki dhidi ya  Algeria.

Magoli 12 ya Messi katika mwaka 2012 yanajumuisha 'hat-trick' zake mbili za kwanza kwa Argentina, alizofunga dhidi ya Brazil na Sweden.

Kama nyongeza, amefunga 'hat-trick' 19 akiwa na Barcelona, maholi manne katika mechi moja na magoli matano katika mechi nyingine moja.

Kutokana na David Villa kuwa mgonjwa baada ya kuumia vibaya Desemba 2011, Pedro ameibuka kuwa kinara wa mabao katika timu ya taifa ya Hispania. Nyota huyo wa Barcelona alikwenda kibahati kwenye fainali za Euro 2012 kutokana na kiwango chake wakati huo kuwa chini, lakini amefunga mabao saba katika mechi nane za timu ya taifa alizocheza mwaka huu.

No comments:

Post a Comment