Gianluca Rocchi |
Uchezeshaji uliojaa utata wa refa Gianluca Rocchi wakati wa mechi ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya Manchester City na Real Madrid haujaachwa bure na Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) baada ya mwamuzi huyo kutoswa katika orodha ya marefa watakaochezesha mechi za mtoano hatua ya 16-Bora ya michuano hiyo.
Huku Pierluigi Collina akiwa ndiye bosi wa Kamati ya Waamuzi ya UEFA kwa sasa, kamwe Rocchi hakutarajiwa kupona katika panga kali la refa huyo mstaafu aliyejitwalia umaarufu mkubwa enzi zake. Na sasa, Rocchi amepigwa chini pamoja na marefa wengine wawili walioonekana kuchemsha kama yeye ambao ni Tagliavento na Rizzolli.
Licha ya kuondoshwa katika orodha ya marefa watakaochezesha hatua ya 16-Bora ya UEFA, Rocchi pia atashushwa daraja na msimu ujao anawexza kupangwa katika Ligi ya Europa na kamwe siyo tena katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Katika tukio mojawapo la kukumbukwa, Rocchi alipeta faulo ya wazi aliyofanyiwa Ronaldo wakati akiwatoka kwa kasi mabeki wa Man City, tukio lililowashangaza wengi na kuwakasirisha Ronaldo na kocha wake Jose Mourinho walioonekana wakilalamika mfululizo kwa kurusha mikono hewani.
Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 1-1, bao la Real Madrid likifungwa na Karim Benzema aliyeunganisha vyema krosi kali ya Angel Di Maria na wenyeji Man Cioty wakasawazisha kupitia penati iliyowekwa wavuni na Sergio Aguero; adhabi ambayo pia iliambantana na kadi nyekundu kwa beki Alvaro Albeloa wa Real Madrid. Sare hiyo iliivusha Madrid kwa hatrua ya 16-Bora huku Man City ikitolewa rasmi.
No comments:
Post a Comment