Rafael Benitez |
Chelsea wamemteua kocha wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez kuwa kocha wao wa muda hadi kufikia mwishoni mwa msimu huu wa ligi.
Kocha aliyetangulia, Roberto Di Matteo alitimuliwa leo Jumatano (Novemba 21) kufuatia kipigo walichopata cha mabao 3-0 katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
Kuteuliwa Benitez kwa kipindi kifupi kunaweza kuwa ni kwa lengo la kuandaa mazingira kabla mmiliki wa klabu, Roman Abramovich hajamsainisha mwisho wa msimu kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola.
Benitez, 52, anakuwa kocha wa tisa wa Chelsea tangu Abramovich alipoinunua klabu hiyo mwaka 2003.
Taarifa iliyotolea na Chelsea imesema: "Mmiliki na Bodi wanaamini kwamba kuwa na Benitez, tumempata kocha mwenye uzoefu wa kutosha katika soka la kiwango cha juu, mtu ambaye atajiunga na mara moja na kusaidia namna nzuri ya kutimiza malengo ya klabu.
"Mshindi mara mbili wa tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa Ulaya amejiunga nasi akiwa na rekodi ya kuvutia."
Benitez alijiunga Liverpool akitokea Valencia mwaka 2004 na kutwaa mataji ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2005, na pia kufika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2007, kabla hajaondoka Liverpool kwa makubaliano maalum mwaka 2010.
Amekuwa nje ya mchezo wa soka tangu alipotimuliwa na Inter Milan ya Italia Desemba 2010 baada ya kuitumikia kwa miezi sita, licha ya kutwaa mataji mawili ya Kombe la Dunia la Klabu na taji la Italia la Super Cup.
Kesho (Novemba 22, 2012), kocha huyo Mhispania anatarajiwa kukutana rasmi na wachezaji wa Chelsea kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Cobham, kabla ya kuiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza katika mechi yao ya nyumbani Jumapili dhidi ya vinara wa msimamo wa Ligi Kuu ya England, klabu ya Manchester City.
No comments:
Post a Comment