Lucas Podolski akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Montpellier wakati wa mechi yao ya Kundi B la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates, London leo Novemba 21, 2012. |
Jack Wilshere wa Arsenal (kulia) akifunga goli la Arsenal dhidi ya Montpellier wakati wa mechi yao ya Ligi ya Kalbu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, leo Novemba 21, 2012. |
Manchester City wameshindwa kufuzu kwa hatua ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa msimu wa pili mfululizo kufuatia sare ya nyumbani ya 1-1 waliyoipata usiku huu (Novemba 21, 2012) dhidi ya Real Madrid.
Man City walitakiwa kushinda lakini walijikuta wakipelekeshwa mwanzoni mwa mechi na kuruhusu goli la mapema wakati Karim Benzema alipotumia vyema krosi ya Angel Di Maria na kuukwamisha mpira wavuni kuipa Real bao la utangulizi.
Straika Sergio Aguero aliisawazishia Man City kwa penati baada ya mapumziko kufuatia faulo aliyochezewa na Alvaro Arbeloa ambaye alitolewa nje ya uwanja kwa kadi ya pili ya njano kutokakana na kosa hilo.
Real Aguero alikaribia kuipa Man City bao la pili katikati ya kipindi cha pili lakini kipa Iker Casillas akaokoa juu ya mstari wa goli.
Mbali na goli la Benzema, Real pia walipoteza nafasi kadhaa za wazi kuibuka na ushindi mnono, zikiwamo mbili zilizopotezwa na Khedira aliyekuwa amebaki na kipa na nyingine ya Ronaldo aliyobaki pia na kipa lakini shuti lake la mpira wa kubetua likaokolewa juu ya mstari na straika huyo akabaniwa tena wakati alipouwa mpira uliorudi na kupiga shuti lililomparaza Vincent Kompany na kuwa kona.
Matokeo hayo yaliihakikishia Real Madrid nafasi ya kufuzu kwa hatua ya 16-Bora pamoja na Borussia Dortmund, ambao waliishindilia Ajax mabao 4-1 na kubaki kileleni mwa msimamo wa kundi lao la D huku kila timu ikiwa imebakiza mechi moja -- Dortmund wakibakiwa na mechi ya nyumbani dhidi ya Man City na Real Madrid wakimalizia nyumbani pia kwa kucheza dhidi ya Ajax.
Katika mechi nyingine za leo, Arsenal ilijihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya 16-Bora pia kutoka katika kundi lao la B baada ya magoli ya Jack Wilshere na Lukas Podolski kuwapa ushindi 'mtamu' wa nyumbani wa 2-0 dhidi ya Montpellier.
MATOKEO MECHI ZA UEFA LEO J'TANO NOV. 21
Arsenal 2 - 0 Montpellier
Man City 1 - 1 Real Madrid
Zenit 2 - 2 Malaga
Ajax 1 - 4 Dortmund
Anderlecht 1 - 3 AC Milan
Dynamo Kiev 0 - 2 PSG
Porto 3 - 0 Zagreb
Schalke 1 - 0 Olympiakos
No comments:
Post a Comment