Yakbiiiirrrrr....! Sheikh Ponda akihamasisha jambo kwa kuinua mkono wakati akizungumza na waumini wa Kiislamu jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Si katika tukio la leo |
Difenda zilizojaa askari wa FFU zikiwa tayari kwa kazi. Si katika tukio la leo |
Sheikh Ponda akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari |
Mabomu hayo ya machozi yalipigwa katika maeneo ya kuanzia Police Central ambako watu hao walikuwa wakielekea kutaka kuachiwa mara moja kwa Sheikh Ponda, kuelekea Mnazi Mmoja kupitia katika mitaa mbalimbali ya maeneo ya Posta, ukiwamo wa Kitumbini.
Katika maeneo yaliyokumbwa na kadhia hiyo, maduka yalifungwa na watu wengi wameonekana wakiwa na vitambaa na maji waliyokuwa wakiyatumia kufutia machozi.
Hata baada ya umati uliojitokeza kumpigania Sheikh Ponda kutawanyika kufuatia hatua ya polisi kutembeza mabomu ya machozi, bado askari wengi wameonekana wakirandaranda huku na kule katika kile kilichoonekana kuwa ni kuhofia kuwa waumini hao watarudi tena.
Magari ya Polisi yameonekana yakipita kwa kupishana mara kwa mara katika maeneo hayo na abiria tele waliokuwamo kwenye daladala mbalimbali wakitokea 'maofisini' Posta kurejea majumbani kwao walijikuta katika wakati mgumu baada ya kukumbana na adha ya moshi wa mabomu ya machozi, ambayo kwa kawaida huwa hayachagui mtu.
Sheikh Ponda alikamatwa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kauli aliyoitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari kulaani kitendo cha kijana mmoja kukojolea Qur-an tukufu na kusababisha vurugu katika maeneo ya Mbagala ambazo baadaye zilipelekea makanisa kadhaa katika maeneo hayo kushambuliwa.
Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesikika leo akiwataka wananchi kuwa watulivu na kwamba wamefanikiwa kudhibiti watu waliojitokeza kupinga kushikiliwa kwa Sheikh Ponda.
No comments:
Post a Comment