WASHAMBULIAJI wa kiwango cha dunia wa timu ya taifa ya Argentina walikuwa nguzo ya ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Chile usiku wa kuamkia leo, ambao uliwapa wageni tofauti ya pointi kileleni mwa msimamo wakati kundi la Amerika Kusini la kuwania kucheza Kombe la Dunia zikienda mapumziko hadi Machi mwakani.
Lionel Messi na Gonzalo Higuain walifunga mwanzoni mwa kila kipindi, na kufanya jumla ya magoli yao kila mmoja kufikia saba, huku Chile wakipata la kufutia machozi kupitia kwa mtokea benchi Felipe Gutierrez katika dakika ya majeruhi mwishoni mwa mechi.
Wakati Messi akienda kujiandaa na mechi mbili za wiki za kimataifa, mashabiki duniani walikuwa wakimhesabia kama ataweza kufunga magoli 10 ili kuifikia rekodi ya wakati wote inayoshikiliwa na Pele ya kufunga magoli 75 katika mwaka mmoja wa kalenda -- yaani kuanzia Januari hadi Desemba.
Edson Arantes do Nascimento, aliyefahamika zaidi kama Pele, anashikilia rekodi ya kukumbukwa pale alipofunga magoli 75 mwaka 1959, ambapo magoli 66 aliyafunga kwa klabu yake ya Santos na tisa kwa timu yake ya taifa ya Brazil.
Messi alianza kuyapunguza magoli hayo 10 kwa kufunga mawili katika ushindi wa Argentina wa 3-0 dhidi ya Uruguay na juzi dhidi ya Chile akatupia moja.
Nyota huyo amekuwa akisambaratisha rekodi zote zilizo mbele yake na kwa mwaka huu wa kalenda tayari amefunga jumla ya mabao 68, ambapo magoli 56 ameifungia Barcelona na 12 ameifungia timu yake ya taifa ya Argentina na kuzima shutuma kwamba haisaidii timu yake ya taifa.
Kwa ufupi, Messi alivunja rekodi yake mwenyewe mwezi mmoja tu uliopita pale alipofunga mara mbili dhidi ya Getafe, na kuipiku rekodi yake mwenyewe ya kufunga magoli 60 katika mwaka mmoja wa kalenda.
Messi ana mwezi mzima na nusu na mechi kibao za kusaka magoli hayo 7 ya kuifikia rekodi ya gwiji wa wakati wote, Pele.
Messi pia sasa amefunga magoli 16 katika mechi 21 zilizopita za timu yake ya taifa, na jumla amefikisha magoli 31 ambapo sasa amebakisha magoli matatu tu kumfikia gwiji wa Argentina Diego Maradona.
Nchini Ureno, goli la dakika za lala-salama kutoka kwa Helder Postiga liliiokoa Ureno kutoka katika kipigo cha kufadhaisha katika usiku ambao Cristiano Ronaldo alikuwa akicheza mechi yao ya 100 kwa timu yake ya taifa wakati walipolazimisha sare ya 1-1 nyumbani didi ya Ireland Kaskazini katika mechi ya Kundi F la kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia jana usiku.
Winga wa klabu ya Aberdeen ya Scotland, Niall McGinn aliwapa Wa-Ireland uongozi usitarajiwa mjini Oporto wakati alipoitumia vyema shambulizi la kustukiza la kasi kubwa katika dakika ya 30.
Postiga kisha akasawazisha dakika 11 kabla ya mechi kumalizika katika uwanja uliojaa mvua kwenye Uwanja wa Dragao.
Ureno sasa ni wa tatu katika kundi hilo, wakiwa na pointi 7 sawa na Israel walio katika nafasi ya pili baada ya mechi nne lakini wako nyuma kwa pointi tano kutoka vinara Urusi. Ireland wana pointi mbili kutokana na mechi tatu na wanashika nafasi ya tatu kutoka mkiani.
MUHTASARI WA MATOKEO YA MECHI ZA KUWANIA KUFUZU KWA KOMBE LA DUNIA ULAYA MECHI ZILIZOCHEZWA JANA USIKU:
Kundi A
Ubelgiji 2 Scotland 0
Uwanja wa King Baudouin mjini Brussels.
Wafungaji: Christian Benteke 69, Vincent Kompany 71
Mapumziko: 0-0
Refa: Tom Hagen (Norway)
--------------------------------------------------------------------------------
Macedonia 1 Serbia 0
Imechezwa: Mjini Skopje
Mfungaji: Agim Ibraimi 59pen
Kadi nyekundu: Nenad Tomovic (Serbia) 58
Refa: Bas Nijhuis (Uholanzi)
--------------------------------------------------------------------------------
Croatia 2 Wales 0
Imechezwa mjini Osijek
Wafungaji: Mario Mandzukic 27, Eduardo 58
Mapumziko: 1-0
Refa: Alexandru Tudor (Romania)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi B
Jamhuri ya Czech 0 Bulgaria 0
Imechezwa mjini Prague
Refa: Vladislav Bezborodov (Russia)
--------------------------------------------------------------------------------
Italia 3 Denmark 1
Imechezwa mjini Milan
Wafungaji:
Italia: Riccardo Montolivo 33, Daniele De Rossi 37, Mario
Balotelli 54
Denmark: William Kvist 45
Kadi nyekundu: Pablo Osvaldo (Italia) 46
Mapumziko: 2-1
Refa: Damir Skomina (Slovenia)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi C
Ujerumani 4 Sweden 4
Uwanja wa Olympic mjini Berlin.
Wafungaji:
Ujerumani: Miroslav Klose 8, 15, Per Mertesacker 39, Mesut
Ozil 56
Sweden: Zlatan Ibrahimovic 62, Mikael Lustig 64, Johan
Elmander 76, Rasmus Elm 90+3
Mapumziko: 3-0
Refa: Pedro Proenca (Ureno)
--------------------------------------------------------------------------------
Austria 4 Kazakhstan 0
Imechezwa Vienna
Wafungaji: Marc Janko 24, 63, David Alaba 71, Martin Harnik
90+3
Refa: Jakob Kehlet (Denmark)
--------------------------------------------------------------------------------
Faroe Islands 1 Ireland 4
Imechezwa Torshavn
Wafungaji:
Faroe Islands: Arnbiorn Hansen 68
Ireland: Marc Wilson 47, Jon Walters 52, Pol Johannus
Justinussen 73og, Darren O'Dea 89
Refa: Lorenc Jemini (Albania)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi D
Romania 1 Uholanzi 4
Imechezwa mjini Bucharest
Wafungaji:
Romania: Ciprian Marica 39
Uholanzi: Jeremain Lens 8, Bruno Martens 28, Rafael van
der Vaart 45+1pen, Robin van Persie 85
Mapumziko: 1-3
Refa: Craig Thomson (Scotland)
--------------------------------------------------------------------------------
Andorra 0 Estonia 1
Imechezwa Andorra La Vella
Mfungaji: Andres Oper 56
Mapumziko: 0-0
Refa: Dimitar Meckarovski (Macedonia)
--------------------------------------------------------------------------------
Hungary 3 Turkey 1
Uwanja wa Ferenc Puskas, Budapest
Wafungaji:
Hungary: Vladimir Koman 31, Adam Szalai 50, Zoltan Gera
57pen
Uturuki: Mevlut Erdinc 22
Mapumziko: 1-1
Refa: Daniele Orsato (Italy)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi E
Iceland 0 Switzerland 2
Imechezwa mjini Reykjavik
Wafungaji: Tranquillo Barnetta 66, Mario Gavranovic 79
Refa: Alan Kelly (Ireland)
--------------------------------------------------------------------------------
Albania 1 Slovenia 0
Ilichezwa Tirana
Wafungaji: Odise Roshi 36
Refa: Martin Hansson (Sweden)
--------------------------------------------------------------------------------
Cyprus 1 Norway 3
Imechezwa Larnaca
wafungaji:
Cyprus: Efstathios Aloneftis 42
Norway: Brede Hangeland 44, Tarik El Younoussi 81pen, Joshua
King 83
Mapumziko: 1-1
Refa: Pawel Gil (Poland)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi F
Portugal 1 Ireland Kaskazini 1
Imechezwa Porto
Wafungaji:
Ureno: Helder Postiga 79
Ireland Kaskazini: Niall McGinn 30
Refa: Thorsten Kinhoefer (Ujerumani)
--------------------------------------------------------------------------------
Israel 3 Luxembourg 0
Imechezwa Tel Aviv
Wafungaji: Tomer Hemed 13, 48, Eden Ben Basat 35
Mapumziko: 2-0
Refa: Harald Lechner (Austria)
--------------------------------------------------------------------------------
Russia 1 Azerbaijan 0
Imechezwa Moscow
Wafungaji: Roman Shirokov 84pen
Mapumziko: 0-0
Refa: Aleksandar Stavrev (Macedonia)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi G
Bosnia 3 Lithuania 0
Imechezwa Zenica
Wafungaji: Vedad Ibisevic 29, Edin Dzeko 35, Miralem Pjanic 41
Mapumziko: 3-0
Refa: Miroslav Zelinka (Jamhuri ya Czech)
--------------------------------------------------------------------------------
Latvia 2 Liechtenstein 0
Imechezwa Riga
Wafungaji: Vladimirs Kamess 29, Edgars Gauracs 77
Kadi nyekundu: Daniel Kaufmann (Liechtenstein) 60
Mapumziko: 1-0
Refa: Istvan Kovacs (Romania)
--------------------------------------------------------------------------------
Slovakia 0 Greece 1
Imechezwa Bratislava
Wafungaji: Dimitris Salpingidis 63
Mapumziko: 0-0
Refa: William Collum (Scotland)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi H
San Marino 0 Moldova 2
ImechezwaSerravalle
Wafungaji: Serghei Dadu 72pen, Alexandru Epureanu 78
Refa: Marios Panayi (Cyprus)
--------------------------------------------------------------------------------
Ukraine 0 Montenegro 1
Imechezwa Kiev
Mfungaji: Dejan Damjanovic 45
Aliyekosa penalti: Stevan Jovetic (Montenegro) 80
Refa: Michael Koukoulakis (Greece)
--------------------------------------------------------------------------------
Kundi I
Hispania 1 Ufaransa 1
Imechezwa mjini Madrid
Wafungaji:
Hispania: Sergio Ramos 25
Ufaransa: Olivier Giroud 90+4
Kukosa penalti: Cesc Fabregas (Hispania) 42
Mapumziko: 1-0
Refa: Felix Brych (Ujerumani)
--------------------------------------------------------------------------------
Belarus 2 Georgia 0
Imechezwa Belarus
Wafungaji: Renan Bressan 6, Stanislav Dragun 28
Mapumziko: 2-0
Refa: Robert Schoergenhofer (Austria)
Matokeo na msimamo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia Ukanda wa CONCACAF
MIAMI, Matokeo na misimamo baada ya mzunguko wa mwisho wa mechi za raundi ya tatu ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa Ukanda wa CONCACAF Timu mbili za juu kutoka kila kundi zinasonga mbele kucheza raundi ya mwisho ya kufuzu mwakani. Kundi A United States 3 Guatemala 1 Jamaica 4 Antigua and Barbuda 1 Msimamo: P W D L F A Pts United States 6 4 1 1 11 6 13 Jamaica 6 3 1 2 9 6 10
Guatemala 6 3 1 2 9 8 10 Antigua and Bar 6 0 1 5 4 13 1 Kundi B Costa Rica 7 Guyana 0 Mexico 2 El Salvador 0 P W D L F A Pts Mexico 6 6 0 0 15 2 18 Costa Rica 6 3 1 2 14 5 10
El Salvador 6 1 2 3 8 11 5 Guyana 6 0 1 5 5 24 1 Kundi C Honduras 8 Canada 1 Cuba 1 Panama 1 P W D L F A Pts Honduras 6 3 2 1 12 3 11 Panama 6 3 2 1 6 2 11
Canada 6 3 1 2 6 10 10 Cuba 6 0 1 5 1 10 1
No comments:
Post a Comment