Thursday, October 4, 2012

MASKINI CARLES PUYOL ...! AMESHAVUNJIKA KILA KIUNGO KWA AJILI YA BARCELONA... ALIANZA KUVUNJIKA KIFUPA CHA USO, HALAFU VIKAFUATIA VIFUPA VYA TAYA, PUA, BEGA, GOTI, KIFUNDO CHA MGUU NA SASA KIWIKO CHA MKONO ALICHOVUNJIKA KATIKA UEFA DHIDI YA BENFICA J'NNE!

Nikipangwa katika el clasico Jumapili poa tu... Puyol akiendelea kuugua hospitalini.
Puyol akiwa na kikinga uso wakati alipovunjika kifupa cha taya Agosti, 2012.
Puyol akiwa na 'hogo' la mkono wake wa kushoto alioumia kiwiko cha mkono katika mechi yao dhidi ya Benfica Jumanne.

Naitamani sana mechi ya el clasico Jumapili -- Puyol.

Yalaaaaa....! Puyol akilalamika baada ya kuteguka kiwiko cha mkono katika mechi yao dhidi ya Benfica Jumanne..
Puyol akitolewa kwa machela kuwahishwa hospitali baada ya kuteguka mkono katika mechi yao dhidi ya Benfica Jumanne
BARCELONA, Hispania
Kama kuna mtu ambaye anaweza kutajwa kuwa 'amekunywa maji ya bendera' na kujitolea kila kitu kwa ajili ya mafanikio ya Barcelona ni nahodha wa timu hiyo, Carles Puyol.

Hadi sasa, Puyol tayari ameshavunjika vifupa kwa nyakati tofauti katika uso wake, taya, gotikifundo cha mguu, pua na sasa kiwiko cha mkono alichovunjika Jumanne katika mechi yao ya ugenini ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya waliyoshinda 2-0 dhidi ya Benfica.

Kwa ufupi, Puyol amevunjika karibu katika kila eneo mwilini kwa sababu ya kucheza kwa moyo moyo wake wote, akicheza jihadi katika kila mechi.

Inaelezwa kuwa kujitolea kwake kwa ajili ya Barca hakutamshangaza yeyote ikiwa ataonekana uwanjani na 'hogo' lake Jumapili akicheza katika mechi yao ya 'el clasico' dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Real Madrid -- licha ya ukweli kwamba hilo haliwezekani.

Tatizo la Puyol linatajwa kuwa ni kawaida yake ya kuichukulia kila mechi kuwa ni fainali. Hata mechi ya 'ndondo' dhidi ya timu ya daraja la pili huichukulia kuwa ni kama fainali ya Kombe la Dunia.

Na hicho ndicho kilichomponza Jumanne wakati aliporuka juu kuosha kwa kichwa kona ya Benfica kana kwamba maisha yake yalikuwa hatarini pindi goli lingefungwa mbele yake wakati wakiwa tayari wanatawala mechi, wakiongoza 2-0 na tena zikiwa zimebaki dakika 10 tu kabla ya mechi kumalizika!

Katika tukio hilo, lililomtokea kwenye mechi yake ya kwanza kwake tangu awe nje kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha, Puyol alianguka vibaya na kuteguka kiwiko cha mkono, hivyo atakuwa nje ya kikosi cha Barceolona kwa miezi miwili.

No comments:

Post a Comment