Tuesday, September 4, 2012

TEVEZ ADAI BIFU NA MANCINI LIMEMSAIDIA KUBORESHA KIWANGO CHAKE


Natishaaaa....! Tevez akishangilia bao lakekatika mechi ya Ligi Kuu ya England waliyoshinda 3-2 dhidi ya Southamton.
Bao tena...! Tevez (kulia) akishangilia baada ya 'kutupia' bao katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Chelsea na kutwaa Ngao ya Jamii.  
Dogo huniwezi hata kabisaaa...! Tevez akimtoka Obi Mikel katika mechi yao ya kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea.
Bye byeeee...! Tevez akiwaacha Onuoha (kushoto) na Bosingwa  wa QPR katika mechi yao ya Ligi kuu ya England juzi. Kwenye mechi hii Tevez alifunga bao katika ushindi wao wa 3-1. 
Tevez (kushoto) akishangilia baada ya kuwapiga bao QPR
BUENOS AIRES, Argentina
CARLOS Tevez anaamini kwamba mgogoro wake na kocha Roberto Mancini msimu uliopita umemsaidia kucheza kwa kiwango cha juu msimu huu katika klabu yake ya Manchester City.

Muargentina huyo alitumia miezi sita akiwa nje ya kikosi cha Man City na kuonekana akikaribia kuondoka baada ya Muitalia Mancini kumtuhumu kuwa alikataa kuingia akitokea benchi wakati wa mechi waliyochapwa ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Mwishowe aliomba radhi na kurejea kikosini, akiisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, na msimu huu amerudi tena kwa kishindo, akionekana kuwa ‘fiti’ zaidi na kucheza katika kiwango cha juu huku akifunga katika kila mechi kati ya nne walizocheza hadi sasa.
Tevez amewaambia waandishi wa habari, kuelekea wiki ndefu ya kuwapo Argentina kwa kusema: "Mgogoro wangu na Mancini ulikuwa na manufaa kwangu.

"Nafurahia tena soka na hicho ndicho kitu ninachokitaka, kujihisi kuwa na usongo wa kuwania mataji na kuwa mwenye furaha kiasi hiki. 

"Nilikuwa na maandalizi safi ya msimu ambayo sijawahi kuwa nayo kwa muda mrefu. Nilijifua sana, najihisi vizuri uwanjani , mwepesi, mwenye nguvu na kasi."

No comments:

Post a Comment