Nicki Minaj (kushoto) na mgombea urais wa Marekani, Mitt Romney |
RAPA wa lebo ya kurekodi muziki ya Young Money, Nicki Minaj kwa mara nyingine amekuwa kitovu cha utata.
Katika wimbo wake mpya wa "Mercy" aliouweka katika albam ya nyimbo mchanganyiko ya Lil Wayne iitwayo 'Dedication 4,' Nicki Minaj anarap: "Mimi ni Republican nampigia kura Mitt Romney, nyie mal*ya wavivu anaua uchumi."
Mstari huu haujawafurahisha mashabiki wa wote Nicki Minaj na Rais Obama.
Tangu kutoka kwa taarifa ya wimbo huo, Nicki Minaj amekuwa mjadala mkubwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter, huku maelfu ya mashabiki wenye hasira waki-tweet kutokuwa na imani na rapa huyo.
Nicki Minaj jana alikuwa na usiku mzuri jana baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya Muziki katika tamasha la MTV Music Awards 2012.
No comments:
Post a Comment