Tuesday, September 11, 2012

MESSI APIGIWA KAMPENI MAGAZETINI PERU AZOMEWE "RONALDO, RONALDO" KUMCHANGANYA AVURUNDE MECHI NA PERU

Lionel Messi

NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amevamiwa na mashabiki waliokuwa wakimzoea kwa kutaja jina la mpinzani wake "Cristiano, Cristiano" nchini Peru wakati akijiandaa kuichezea Argentina dhidi ya Peru alfajiri ya kesho.

Wakati kikosi cha Argentina kilipotua mjini Lima, mashabiki wa Peru walianza kuimba jina la nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo wakati walipomuona Messi katika uwanja wa ndege wa nchi hiyo.

Vyombo vya habari vya Peru vilidhamiria kumvuruga kichwa Messi na viliwaomba mashabiki kuimba 'Cristiano, Cristiano' popote watakapomuona mchezaji huyo kuelekea katika mechi hiyo iliyopigwa leo saa 10:25 usiku.

Katika habari nyingine, Barcelona wanadhamiria kukaa na Messi na kujadili mkataba mpya ulioboreshwa katika wiki chache zijazo.

Gazeti la El Mundo Deportivo limesema pande zote hazijazungumzia mkataba wa Messi tangu mwaka 2009, wakati aliposaini mkataba wa miaka saba utakaomalizika mwaka 2016.

Tangu wakati huo, Messi ameshinda tuzo tatu mfululizo za Ballon d'Or za Mwanasoka Bora wa Dunia Mwaka na pia "Sheria ya Beckham" imefutwa - ambayo ilikuwa ikiwaepushia wanasoka na kodi kubwa ya asilimia 56.

Barca wanataka kuboresha mkataba wa Messi na pia kuongeza muda wake wa kuichezea klabu hiyo uwe ni "maisha".



No comments:

Post a Comment