Andres Iniesta |
BARCELONA,
Hispania
Andres Iniesta
na Jordi Alba walirejea kutoka katika majukumu ya kuichezea timu ya taifa lao
wakiwa na majeraha na maradhi licha ya kwamba wote walicheza kwa dakika zote 90
wakati wakiisaidia Hispania kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Georgia
Jumanne usiku.
Iniesta
aliumia msuli wa katikati ya goti na paja la mguu wa kulia na madaktari wa
Barcelona wamethibitisha kuwa atakuwa nje kwa siku 10-15.
Kiungo huyo hatakuwamo katika kikosi cha timu yake kitakachocheza keshokutwa Jumamosi mechi
ya ugenini ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Getafe na ya nyumbani
dhidi ya Granada. Atakosa pia mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya
Barcelona na Spartak Moscow itakayopigwa Jumatano.
Jordi
Alba yuko shakani pia kucheza keshokutwa dhidi ya Getafe, lakini hajaondolewa
katika kikosi kitakachokuwa Madrid kucheza mechi hiyo.
No comments:
Post a Comment