Abou Diaby |
KIUNGO wa timu ya taifa ya Ufaransa, Abou Diaby yuko hatarini kukosa mechi ya kesho ya Kundi I la hatua za awali kuwania kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia dhidi ya Belarus baada ya kuumia Ijumaa.
Diaby, aliyeifungia Ufaransa bao pekee la ushindi Ijumaa dhidi ya Finland, amepata jeraha la kuumia msuli na hivyo yuko hatarini kucheza mechi ya kesho kwenye dimba la Stade de France.
"Aliumia vibaya (dhidi ya Finland) na hakushiriki mazoezi ya leo," kocha Didier Deschamps aliuambia mkutano na waandishi wa habari leo, akiongeza kwamba beki Gael Clichy pia amejeheruhiwa.
"Wote hawana uhakika wa kuanza kikosini."
Diaby amekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara. Aliichezea Arsenal katika mechi nne tu msimu uliopita na kukosa fainali za Euro 2012.
Deschamps amesema straika mpya wa Arsenal, Olivier Giroud, aliyekosa mechi yao dhidi ya Finland, amepona lakini hakuthibitisha kama atampanga kesho.
No comments:
Post a Comment