Sunday, August 26, 2012

YOSSO REAL MADRID WAWAFUNGA YOSSO WENZAO WA BARCELONA 3-2 KATIKA ‘EL CLASICO’ YAO YA SEGUNDA B


Juanfran wa Real Madrid Castilla (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Barcelona B wakati wa mechi yao ya Segunda B kwenye Uwanja wa Alfredo Di Stefano jana.
Gooooohhh...! Yosso Denis wa Real Madrid akishangilia baada ya kufunga goli katika mechi yao dhidi ya Barcelona B jana.

Mwakani ntamwambia Mourinho awasajili... Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez (mwenye miwani katikati) akifuatilia mechi ya 'el clasico' ya yosso wa timu yake dhidi ya Barcelona B kwenye Uwanja wa Alfredo Di Stefano jana. 
Nipishe huko...! Kama Angel Di Maria vile. Yosso wa Real Madrid akijaribu kuwatoka mabeki wa Barcelona B wakati wa mechi yao ya Segunda B jana.
Mourinho umeniona?
Mabao ya Juanfran, Denis na jingine la kujifunga kutoka kwa Sergi Gómez yaliipa timu ya yosso wa Real Madrid (Castilla) ushindi ‘mtamu’ wa nyumbani wa mabao 3-2 dhidi ya wenzao wa Barcelona B katika mechi yao ya ‘el clasico’ ya Segunda B, Ligi Daraja la Kwanza Hispania iliyochezwa anza jana.

Mechi hiyo iliyojaza maelfu ya mashabiki kutokana na mvuto wake, ilichezwa kwenye uwanja wa Real Madrid Castilla uitwao Alfredo Di Stefano.
Real Madrid Castilla na Barcelona B ndio timu pekee za vikosi vya pili vya klabu za La Liga, Ligi Kuu ya Hispania zinazoshiriki Segubnda B msimu huu, na zimekutana jana kwa mara ya kwanza katika ligi hiyo baada ya kupita miaka 15.
Mara ya mwisho zilipokutana mara nne kwenye Segunda B, ilikuwa ni katika misimu ya 1995/96 na 1996/97, ambapo timu ya yosso wa Real Madrid ilishinda zote.
Jana,  Castilla walianza kupata bao la utangulizi katika dakika ya 10 baada ya Álex kupiga krosi safi iliyopokewa na Juanfran aliyetuliza kifuani kabla ya kumzidi Oier na kupiga shuti lililojaa wavuni.

Denis akaifungia Castilla bao la pili katika dakika ya 24.  Mejías alijifunga katika dakika ya 38 na kuwapatia Barcelona B bao la kwanza. Krosi ya Juanfran katika dakika ya 46 ilimbabatiza beki Sergi Gómez na kutinga wavuni, hivyo kuipa Castilla uongozi wa mabao 3-1. Katika dakika ya 69, Barcelona B walipata bao la pili kupitia penati iliyopigwa na Sergi Roberto baada ya Balliu kuangushwa ndani ya eneo la 18.

No comments:

Post a Comment