MADRID, Hispania
Bao la kichwa alilofunga Cristiano Ronaldo Alhamisi dhidi ya Barcelona katika mechi ya kwanza ya 'el clasico' kwenye Uwanja wa Nou Camp kuwania taji la Super Cup limemuongezea rekodi kwa kuwa mchezaji pekee wa Real Madrid kuwahi kuitungua Barca nyumbani kwao katika mechi nne mfululizo.
Rekodi hiyo imumweka Ronaldo kileleni mwa wakali kibao waliowahi kupita Real Madrid wakiwamo magwiji kama Di Stefano, Zinedine Zidane 'Zizzou', Ronaldo De Lima na hata Mreno mwenzake Luis Figo.
Ronaldo aliidungua Barca Agosti mwaka jana katika mechi ya Super Cup, akawatandika tena Januari, 2012 katika mechi ya marudiano ya Kombe la Mfalme, April, 2012 akapiga goli 'kali' la ushindi wakati Real iliposhinda 2-1 katika marudiano ya mechi ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania msimu uliopita na Alhamisi iliyopita, akafunga tena wakati wakilala 3-2 katika mechi ya kwanza ya taji la Super Cup la Hispania.
Real Madrid watarudiana na Barcelona kuwania taji la Super Cup Jumatano kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
No comments:
Post a Comment