Xabi Alonso |
MADRID, Hispania
KUNA taarifa zilizopatikana leo zinazodai kuwa kiungo Xabi Alonso ametishia kutofanya mazungumzo
ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu yake ya Real Madrid.
Gazeti la Sport limesema kwamba
sasa Xabi anafikiria kuhitimisha kipindi chake cha kuichezea Real baada ya
kumalizika kwa msimu ujao.
Mkataba wa sasa wa kiungo huyo
mchezeshaji aliyewahi kuichezea pia Liverpool unamfunga Real hadi mwaka
2014 na licha ya kufurahia maisha kwa vigogo hao wa Hispania, lakini anaamini
kwamba sasa kipindi chake cha kung'ara kwenye klabu hiyo kinaelekea ukingoni.
Juventus na Inter Milan zimedaiwa
kuanza kufuatilia kwa karibu maendeleo ya mazungumzo ya nyota huyo wa timu ya
taifa ya Hispania na klabu yake ili ikibidi zianze harakati za kumtwaa.
No comments:
Post a Comment