Van Persie |
Santi Carzola... mmoja wa nyota wapya wa Arsenal wanaodaiwa kumvutia Van Persie na kumfanya afikirie mara mbili uamuzi wake wa kutaka kuondoka. |
Lucas Podolski... mkali mwingine aliyesajiliwa na Wenger hivi karibuni. |
Nuri Sahin.... kiungo huyu nyota anatarajiwa kutua Arsenal kutoka Real Madrid. Inaelezwa kuwa ujio wake pia unamshawishi Van Persie kutaka kubaki Arsenal. |
NAHODHA wa Arsenal, Robin van Persie ameungana na wachezaji wenzake wa klabu ya Arsenal kwenda Ujerumani kujifua kwa
ajili ya msimu ujao huku hatma yake katika klabu hiyo bado ikiwa njiapanda.
Straika huyo, ambaye alishatangaza
dhamira yake ya kutaka kuondoka Arsenal katika barua ya wazi aliyowaandikia
mashabiki wa klabu hiyo mwezi uliopita, alikwea pipa na wachezaji wenzake na
pia kocha Arsene Wenger jana na kwenda Ujerumani wanakotarajiwa kucheza mechi
ya kirafiki dhidi ya Koln mwishoni mwa wiki.
Mholanzi huyo amezivutia klabu za Juventus,
Manchester City na Manchester United baada ya kuhoji hadharani malengo ya klabu
hiyo Julai 4, kufuatia Arsenal kumaliza msimu wa saba mfululizo bila kutwaa
taji lolote, na pia msimu uliopita kumaliza ikiwa nyuma ya Man City na Man U kwa
pointi 19.
Hata hivyo, imebainika kwamba Van
Persie amefurahishwa na usajili wa nyota kutoka Malaga, Santi Cazorla na pia
jitihada za kumleta kiungo Nuri Sahin kutoka Real Madrid, hivyo anaelekea
kubadili uamuzi wake wa kutaka kuhama na badala yake kuungana na wenzake katika
mazoezi ya kujiandaa na msimu.
Olivier Giroud na Lukas Podolski, ambaye
anaweza kucheza dhidi ya timu yake ya zamani katika mechi ya kirafiki ya
Jumapili kwenye Uwanja wa RheinEnergie, tayari walishasajiliwa na Wenger wakati
wa dirisha la usajili unaoendelea wa majira ya kiangazi.
No comments:
Post a Comment