Danny Welbeck |
Robin Van Persie akishangilia goli lake la pili dhidi ya Sunderland England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Oktoba 16, 2011. Picha: REUTERS |
DANNY Welbeck amebashiri kwamba msimu huu Manchester United itanyeshea wapinzani wao "mvua za magoli".
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya England huenda akapoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza kutokana na kuwasili kwa mshambuliaji anayefunga mabao bila ya "breki" Robin van Persie aliyesajiliwa kwa paundi milioni 22 kutoka Arsenal.
Lakini alisema: "Robin ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa sana na nimshambuliaji wa kiwango cha dunia.
"Anaweza kufuga magoli na kupikia wenzake nafasi za kufunga. Wao ni aina ya wachezaji wanayokusaidia kutwaa mataji.
"Ni bonge la usajili kwa klabu yetu, kila mmoja amefurahi. Ninajiandaa kucheza pamoja naye."
Welbeck (21) aliongeza: "Hapa Man United unajifunza kucheza na aina tofauti za washambuliaji na wachezaji.
"Tutakapoanza kufanya mazoezi pamoja nadhani kila mtu tunatengeneza ushirikiano baab'kubwa — itakuwa ni mvua za magoli tu kwa Manchester United."
No comments:
Post a Comment