Theo Walcott |
Theo Walcott wa Arsenal akimtoka beki mmojawapo wa Kitchee FC wakati wa mechi yao ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya kwenye Uwanja wa Hong Kong, Julai 29, 2012. |
KLABU ya Arsenal bado inahaha katika mazungumzo yanayoendelea hadi leo ya kujaribu kumshawishi straika Theo Walcott asaini mkataba mpya utakaofuta uvumi wa kuhama kwake.
Imeelezwa kuwa straika huyo wa timu ya taifa ya England anauchanganya uongozi wa Arsenal kwani hadi sasa bado hajakubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumuikia timu hiyo kaskazini mwa jiji la London.
Gazeti la The Sun limesema kwamba hofu imetawala miongoni mwa viongozi wa Arsenal kuwa straika huyo atakuwa mchezaji mwingine mwenye jina kubwa kuiacha timu hiyo katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi baada ya nahodha wao wa zamani, Robin van Persie kuhamia Manchester United.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwepo kwa hofu ya kumpoteza Walcott na kusema: “Bado tunajaribu kuzungumza naye ili kuongeza mkataba wake.”
Kabla ya kuiacha Arsenal na jana kusaini mkataba wa miaka minne kuichezea Man U, Van Persie pia alikataa kusaini mkataba mpya wa kumuongezea kubaki katika klabu yake ya zamani.
No comments:
Post a Comment