Friday, August 10, 2012

ROONEY: VAN PERSIE ATATISHA SANA AKIJA KWETU MAN U

Van Persie

Van Persie a.k.a Van Magoli! Akiungana kweli na Rooney, Man U si itatisha zaidi kwa kuwa na safu hatari ya mastraika England?
Wayne Rooney... anamfagilia Van Persie ili washirikiane naye kupioga magoli kama mvua, sivyo? Hapa yeye akishangilia baada ya kupiga goli katika mechi mojawapo ya msimu uliopita.
LONDON, England
STRAIKA Wayne Rooney amemwagia sifa Robin van Persie waArsenal wakati klabu yake ya Manchester United ikipania kuendelea kumshawishi straika huyo ajiunge nao katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Mholanzi huyo alifichua mwezi uliopita kwamba hatasaini mkataba mpya wa kuichezea Arsenal, akitoa sababu ya kutoridhisha na "mipango ya kuiendeleza Arsenal." Uvumi kuhusiana na hatma yake ulianza kushika kasi tangu alipoweka hadharani msimamo wake huo.

Ingawa Van Persie hakuwamo katika ziara ya Arsenal barani Asia, alikwea pipa Jumatatu kwenda Ujerumanikujiunga na wenzake katika wiki ndefu ya kujifua kwa maandalizi ya msimu, hivyo kuonekana kama amesitisha kusudio lake la kutaka kuhama.

Pamoja na hayo, Rooney alijawa na furaha kuhusiana na taarifa za uwezekano wa klabu yake kumsajili nahodha huyo wa Arsenal.

"Ni wazi kwamba yeye ni mchezaji anayenivutia," Rooney aliiambia Daily Mail. 


"Ni mchezaji safi sana, amekuwa akionyesha kiwango cha juu akiwa na Arsenal kwa miaka mingi. Msimu uliopita unaweza ukawa ndio msimu bora zaidi kwake, alifunga magoli mengi sana.

"Kama atajiunga nasi ataongeza sana makali kikosini."

Alipoulizwa kama anaweza kucheza pamoja na Van Persie, Rooney aliongeza: "Ningetamani jambo hilo -- lakini mnapaswa kumuuliza kocha.

"Tayari tuna washambuliaji wengi hapa wakiwemo mimi mwenyewe, (Danny) Welbeck, Chicharito na (Dimitar) Berbatov, na sote tunaweza kucheza. Kwa hiyo kuna washambuliaji wengi wanaopigania namba."

Kocha Alex Ferguson alithibitisha juzi kwamba Man U wametuma maombi ya kumsajili Van Persie lakini akafichua kwamba hakuna jibu lolote walilopewa na Arsenal.

No comments:

Post a Comment