Hee...! Nini tena? Van Persie na mkewe Bouchra wakicheza ndani ya maji |
Chu-chu-chuuu...! Van Persie akicheza majini na binti yake, Dina kwenye visiwa vya Pitiusic, mwaka juzi. |
Angalia kuleee....! Van Persie akipata maelekezo kutoka kwa mkewe Bouchra kwenye visiwa vya Pitiusic, mwaka juzi. |
Fumba macho...! Van Persie akimsikiliza mkewe Bouchra huku pembeni wakiwa na mpambe aliyembeba mtoto wao wa kiume, Shaquille. Hii ilikuwa mwaka juzi |
Bouchra... mke wa Van Persie |
Mmmmwaaaa... ndio kuna mtoto lakini hayakuhusu!! |
Van Persie akiwa na binti yake, Dina katika fukwe za visiwa vya Pitiusic |
Daddy nishushe... Van Persie na binti yake Dina wakiwa kwenye fukwe za visiwa vya Pitiusic, Julai 14, 2012 |
Taratibu...! |
Safari imeanza... Van Persie, mkewe Bouchra na watoto wao Shaquille na Dina wakiwa ndani ya boti ndogo kwenye fukwe za visiwa vya Pitiusic, Julai 14, 2012 |
Lazima niondoke Arsenal...Van Persie akionekana mtulivu wakati yeye na familia yake wakiponda maraha kwenye visiwa vya Pitiusic, Julai 14, 2012 |
Hapa ni Van Persie, familia yake na wapambe.... ndani ya boti kwenye visiwa vya Pitiusic, Julai 14, 2012 |
Van Persie na mkewe Bouchra |
Twenzetu...! Van Persie na mkewe Bouchra wakiwa tayari kwa mtoko |
Wakati akiwa akiichezea klabu ya Arsenal, Robin van Persie alikuwa amejenga mazoea ya kuambatana na familia yake kwenda kuponda maraha katika visiwa vya Pitiusic vilivyopo nchini Hispania.
Kila alipokuwa katika mapumziko marefu ya msimu, Van Persie na familia yake hawakuwa wakijiweka nyuma. Walikwenda sehemu mbalimbali zenye utulivu na kujiachia kiasi cha kutosha.
Karibu nusu ya mwezi ulipita, straika huyo aliyekamilisha uhamisho wa kwenda Manchester United akitokea Arsenal kwa ada ya paundi za England milioni 24 (Sh. bilioni 60), aliongozana na mkewe Bouchra na watoto wao Shaquille na Dina kwenda kufaidi maisha katika fukwe za visiwa hivyo vya Pitiusic, wakiambatana pia na swahiba zao kadhaa.
Van Persie na familia yake walionekana ufukweni wakitabasamu muda wote; wakila, kunywa, kuchezea maji na kujianika juani kadri walivyotaka.
Uhamisho wa kwenda Man U mwishoni mwa wiki umemhakikishia 'mafweza' zaidi mifukoni mwake na pengine kuwafanya mkewe na wanawe wafaidi zaidi maisha; kwani imeelezwa kuwa katika mkataba wake wa miaka minne, sasa straika huyo wa kimataifa wa Uholanzi atakuwa akilipwa mshahara mnono wa paundi za England 250,000 kwa wiki, sawa na Sh. milioni 615!
Je, kwanini Van Persie na familia yake wasiendelee kufaidi maisha katika maeneo ghali kama ya visiwa vya Pitiusic?
No comments:
Post a Comment