Saturday, August 4, 2012

MICHAEL PHELPS ASHINDA DHAHABU YA TATU LONDON, AFIKISHA MEDALI 21 OLIMPIKI

Michael Phelps

MICHAEL Phelps alipata medali yake ya tatu ya mshiriki mmoja mmoja  kabla ya kustaafu, baada ya shindani la kuogelea la kwa mtindo wa kipepeo mita 100.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 27 kuzinduka kwake mwishoni kumempatia medali yake ya tatu ya dhahabu katika Michezo ya Olimpiki ya London 2012 na kufanya jumla ya medali zote alizoshinda katika Olimpiki kuwa 21.

Waogeleaji wa Afrika Kusini, Chad Le Clos na Evgeny Korotyshkin wote waligusa ukuta kwa pamoja jambo lililowafanya wafungane katika kupewa medali ya fedha.

"Ilikuwa ni njia nzuri ya kumalizia shindano langu la mwisho kabisa la kuogelea maishani mwangu," alisema Phelps.

"Sikumaliza vizuri na sikugeuka vizuri lakini nina furaha kwa kuwa nimetetea taji langu."

Phelps, ambaye ashinda medali yake ya kwanza ya dhahabu ya mshiriki mmoja-mmoja kwa kumshinda Ryan Lochte katika mita 200, hivi sasa ana jumla ya dhahabu tano za michuano ya London 2012 ukijumlisha na za kuogelea kwa timu.

No comments:

Post a Comment