Saturday, August 4, 2012

BOLT, BLAKE, GAY KUCHUANA MCHUJO SAA 8:30 LEO


WATU wenye kasi zaidi duniani akiwemo Usain Bolt, Yohan Blake, Gay, Gatlin, Powell na Gemili, watachuana katika mbio za mchujo za mita 100 zitakazofanyika leo saa 8:30 mchana yaani dakika chache kutokea sasa.

PICHANI: Muunganiko wa picha zinazowaonyesha wanariadha wenye kasi zaidi ambao watachuana katika fainali za mbio za mita 100 za Michezo ya Olimpiki ya London 2012 kesho Agosti 5, 2012. Kutoka kushoto mstari wa juu ni Wajamaica Usain Bolt, Asafa Powell and Yohan Blake. Mstari wa katikati kutoka kushoto ni Justin Gatlin na Tyson Gay wa Marekani. Mstari wa chini kutoka kushoto ni Keston Bledman (Trinidad na Tobago), Christophe Lemaitre wa Ufaransa Ryan Bailey wa Marekani. Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 116, mbio za Olimpiki za mita 100 zimekuwa zikileta ushindani mkubwa, machungu, utata, fadhaa, maajabu na furaha isiyomithilika - yote hayo yakipatikana katika mbio hizo ambazo humalizika mapema zaidi muda utakaoutumia kutamka neno "Baron Pierre de Coubertin." Picha: RE
UTERS

No comments:

Post a Comment