Thursday, August 16, 2012

MESSI, RONALDO WAFUNGA MAGOLI, ARGENTINA, URENO ZIKIUA, SHABIKI AVAMIA UWANJANI KUMPA MESSI ZAWADI YA UA

Muunganiko wa picha nne zinazomuonyesha shabiki aliyevamia uwanjani kwa ajili ya kumpa zawadi ya ua mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Ujerumani mjini Frankfurt Agosti 15, 2012. Argentina ilishinda 3-1. Picha: REUTERS
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo (kushoto) akijaribu "ku-kontroo" mpira jirani na mchezaji wa Panama, Roman Torres wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Algarve jirani na Faro usiku wa kuamkia leo. Ureno walishinda 2-0. Picha: REUTERS
Winga wa Ureno, Nani akikimbia na mpira jirani na mchezaji wa Panama, Luis Henriquez (kushoto), Carlos Cedeno (wa pili kulia) na Carlos Rodriguez (kulia) wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Algarve jirani na Faro usiku wa kuamkia leo. Ureno walishinda 2-0. Picha: REUTERS
Winga wa Ureno, Nani (17) akimpongeza Cristiano Ronaldo (7) baada ya kufunga goli wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Algarve jirani na Faro usiku wa kuamkia leo. Ureno walishinda 2-0. Picha: REUTERS
Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo akijilaumu baada ya kupoteza nafasi ya kufunga dhidi ya Panama wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Algarve jirani na Faro usiku wa kuamkia leo. Ureno walishinda 2-0. Picha: REUTERS

Mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo akijilaumu baada ya kupoteza nafasi ya kufunga dhidi ya Panama wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Algarve jirani na Faro usiku wa kuamkia leo. Ureno walishinda 2-0. Picha: REUTERS

Romelu Lukaku (kulia) wa Ubelgiji akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Uholanzi wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa King Baudouin mjini Brussels usiku wa kuamkia leo. Ubelgiji iliifunga Uholanzi 4-2. Picha: REUTERS

Shabiki wa soka akimpa mkono mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi (kushoto) baada ya kuvamia uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Ujerumani mjini Frankfurt usiku wa kuamkia jana. Argentina ilishinda 2-1. Picha: REUTERS
Wachezaji wa Argentina wakishangilia baada ya kushinda mechi yao ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Ujerumani mjini Frankfurt usiku wa kuamkia jana. Argentina ilishinda 2-1. Picha: REUTERS
Romelu Lukaku wa Ubelgi (kulia) akimuangalia kipa Maarten Stekelenburg wakati akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Uholanzi wakati wa mechi yao ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa King Baudouin mjini Brussels usiku wa kuamkia leo. Ubelgiji iliifunga Uholanzi 4-2. Picha: REUTERS
Mshambuliaji wa England, Jermain Defoe (19) na wachezaji wenzake wakishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Italia wakati wa mechi yao ya kirafiki mjini Bern, Uswisi usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS


Mshambuliaji wa England, Jermain Defoe akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Italia wakati wa mechi yao ya kirafiki mjini Bern, Uswisi usiku wa kuamkia leo. Picha: REUTERS
Mshambuliaji wa Brazil, Pato (katikati), Dani Alves (kushoto) na Hulk akishangilia baada ya Alves kufunga goli wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Sweden kwenye Uwanja wa Rasunda mjini Stockholm jana usiku Agosti 15, 2012. Brazil ilishinda 3-0. Picha: REUTERS

LONDON, Uingereza
LIONEL Messi alifunga goli moja na kukosa penalti katika ushindi wa Argentina wa 3-1 ugenini dhidi ya Ujerumani wakati Ubelgiji iliishangaza Uholanzi kwa kipigo cha 4-2 wakati makocha wapya na wachezaji waliokuwa wakizichezea timu zao za taifa kwa mara ya kwanza katika mechi za kimataifa jana.

Huku mechi za kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2014  zikikaribia Septemba, Didier Deschamps alianza kichovu kama kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa kwa sare ya 0-0 dhidi ya Uruguay na mechi ya kwanza ya Fabio Capello kama kocha wa Urusi iliisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya Ivory Coast. 

Mabingwa wa dunia na na Ulaya Hispania, ambayo walichezesha kikosi ngangari ambacho hakikutarajiwa, walishinda 2-1 ugenini Puerto Rico kupitia magoli yaliyopatikana kabla ya mapumziko kutoka kwa Santi Cazorla na Cesc Fabregas, ingawa Juanfran alitoka akichechemea baada ya kuumia.

England walilipa kisasi cha kufungwa na Italia kwenye Euro 2012 kwa kuwachapa 2-1 mjini Berne shukrani kwa goli kali la ushindi kutoka kwa Jermain Defoe na Brazil walisahau machungu ya kufungwa katika fainali ya Olimpiki kwa ushindi wa 3-0 ugenini Sweden, huku Alexandre Pato akifunga magoli mawili ya dakika za lala salama.

Ureno iliifunga Panama 2-0 huku Cristiano Ronaldo akifunga goli kali la pili.

Louis van Gaal alirejea vibaya katika benchi la ufundi la Uholanzi wakati washindi hao wa pili wa Kombe la Dunia, ambapo "walifulia" katika Euro 2012 na kusababisha kujiuzulu kwa kocha Bert van Marwijk, walizinduka kutoka nyuma na kuongoza, kabla hawajalala mikononi mwa majirani zao Ubelgiji mjini Brussels.

"Madhambi aliyochezewa Nigel de Jong (wakati Ubelgiji wakielekea kufunga goli lao la pili) ilikuwa na mchango mkubwa katika utawala wao na si tu kwamba walipata goli la kusawazisha bali pia liliwarejesha Ubelgiji mchezoni," Van Gaal told SBS6-TV.

Marc Wilmots alifurahia mechi yake ya kwanza kama kocha mpya wa Ubelgiji, ambao walikosa fainali za Euro 2012 lakini waliojaza vipaji na kupata goli la kuongoza kupitia kwa Christian Benteke.

Luciano Narsingh na Klaas Jan Huntelaar wakaifungia Uholanzi baada ya mapumziko na kuinua matumaini ya Van Gaal, kabla ya Dries Mertens, Romelu Lukaku na Jan Vertonghen kuipa Ubelgiji ushindi.

Bingwa wa majukumu magumu Van Gaal, ambaye aliifundisha Uholanzi kwa mara ya mwisho mwaka 2002, sasa ni lazima aipike upya timu hiyo maarufu kama "Oranje" kwa ajili ya mechi yao ya Sept. 7 ya Kundi D la kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia nyumbani dhidi ya Uturuki, ambao walilala 2-0 nchini Austria.

Mechi za kirafiki za mwezi huu, zilizofanyika kabla ya kuanza kwa ligi nyingi za Ulaya, zilipingwa na makocha wengi wa klabu na watafurahishwa kusiia kwamba zitafutwa katika miaka ijayo.

Wachezaji wengi vinara walijitoa katika mechi hizo za kirafiki wakisema hazina maana, wakati kulikuwa na mvuto hafifu katika baadhi ya majukwaa huku mechi ya England dhidi ya Italia ikihudhuriwa na mashabiki nusu uwanja njini Berne.

Sababu ya kucheza hiyo kwenye uwanja usiohusisha upande wowote nchini Uswisi zilikuwa nje ya uwezo wa mashabiki wengi  lakini makocha Cesare Prandelli na Roy Hodgson angalau walipata fursa ya kuwapima yosso wao.

Italia, ambayo iliifunga England kwa penalti katika robo fainali ya Euro 2012 kabla ya kufungwa na Italia katika fainali, waliwaanzisha kwa mara ya kwanza washambuliaji Mattia Destro na Stephan El Shaarawy lakini alikuwa ni nyota wa zamani Daniele De Rossi aliyefunga goli katika dakika ya 15.

KICHWA CHA MBIZI
Kipa wa England, Jack Butland, ambayr hajawahi kucheza Ligi Kuu ya England, angeweza kufanya vyema zaidi katika mechi yake ya kwanza timu ya taifa lakini alifarijika katika dakika ya 27 wakati Phil Jagielka alipofunga goli lake la kwanza la kimataifa kwa "kichwa cha mbizi", kwa mara nyingine ktokana na kona.

Defoe kisha akafunga kwa shuti tamu la upinde wa mvua lililowapa ushindi dakika 10 kabla mechi kumalizika.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England, Capello alifurahia sare ya Urusi lakini aliguswa na tukio la mshambuliaji anayepanda na kushuka kiwango Andrei Arshavin kuzomewa na mashabiki wao wenyewe wakati alipompumzisha.

"Lilikuwa si jambo la kufurahisha kuona mashabiki wakimzomea Arshavin. Mimi sielewi jambo lile," Muitalia huyo aliwaambia waandishi wa habari. "Tulipoteza umakini kutokana na jambo lile na mara moja tukaruhusu goli."

Mjini Frankfurt, Messi alikosa penalti ya kipindi cha kwanza lakini alirekebisha makosa yake kwa goli kali ya kipindi cha pili.

Goli la kujifunga kutoka Sami Khedira liliwapa wageni uongozi, Messi akafunga la pili na Angel Di Maria 'akatupia' la tatu.

Ujerumani ambao goli lao la kufutia machozi lilifungwa na Benedikt Hoewedes, walicheza kwa takriban saa nzima wakiwa 10 baada ya kipa Ron-Robert Zieler kutolewa kwa kadi nyekundu na kutokana na faulo iliyosababisha penalti iliyokoswa.

Mahasimu wao wa Amerika Kusini, Brazil, ambao kama Argentina wako katikati ya mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia, walipata ushindi wa kuongeza morali kwa kocha Mano Menezes baada ya kufungwa isivyotarajiwa katika fainali ya Olimpiki inayohusisha wachezaji wa U-23 dhidi ya Mexico Jumamosi.

Huku Pele akishuhudia kutokea jukwaani katika mechi ya kimataifa kwenye Uwanja wa Rasunda mjini Stockholm, Leandro Damiao aliwapa goli la kwanza Brazil katika kipindi cha kwanza  kabla ya mchezaji wa akiba Pato kufunga kwa kichwa katika dakika ya 85 na kisha kufunga penalti licha ya kuteleza kabla hajaipiga.

Mabingwa wa Afrika, Zambia walilala 2-1 kwa Korea Kusini, Japan walitoka sare ya 1-1 na Venezuela, China walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Ghana, Scotland waliifunga Australia 3-1 na Serbia ilitoka sare ya 0-0 na Ireland.

Miongoni mwa mmechi nyingine, kocha mpya wa Poland, Waldemar Fornalik alikumbana na kipigo cha 1-0 kutoka kwa Estonia, Ukraine walitoka sare ya 0-0 dhidi ya Czech, Ugiriki walishinda 3-2 nchini Norway, Denmark walilala 3-1 nyumbani dhidi ya Slovakia na Uswisi iliwafunga Croatia 4-2.

LONDON, Matokeo ya mechi za kirafiki za kimataifa zilizochezwa juzi Jumatano:
Japan                   1    Venezuela           1
Korea Kusini       2    Zambia               1
China                   1    Ghana                1
Urusi                    1    Ivory Coast        1
Armenia              1    Belarus               2
Azerbaijan           3    Bahrain               0
Niger                   0    Nigeria                0
Tunisia                2    Iran                     2
Oman                  1    Misri                   1
Sweden               0    Brazil                  3
Norway               2    Ugiriki                 3
Ukraine               0    Jamhuri ya Czech      0
Denmark             1    Slovakia               3
Croatia                2    Uswisi                 4
Bulgaria              1    Cyprus                 0
Montenegro        2    Latvia                  0
Hungary              1    Israel                    1
Austria                2    Uturuki                 0
Macedonia         1    Lithuania               0
Ubelgiji               4    Uholanzi               2
Estonia               1    Poland                   0
Ujerumani           1    Argentina              3
Ireland Kask.      3    Finland                  3
Serbia                 0    Ireland                   0
Slovenia             4    Romania                 3
Wales                  0    Bosnia                    2
England               2    Italia                      1 (mjini Berne)
Scotland              3    Australia                1
Ufaransa             0    Uruguay                  0
Albania               0    Moldova                  0
Luxembourg        1    Georgia                  2
Iceland                 2    Visiwa vya Faroe   0
Ureno                   2    Panama                  0
Puerto Rico         1    Hispania                  2       
       

No comments:

Post a Comment