Beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite (katikati) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Seletine Mwesigwa |
Mbuyu Twite (katikati) akisalimia mashabiki baada ya kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. |
Twite akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege |
Mashabiki wenye ngoma wakisubiri kuwasili kwa beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere |
Mamia ya mashabiki waliofurika kumpokea Twite |
Mamia ya mashabiki waliofurika kumpokea Twite |
Mamia ya mashabiki waliofurika kumpokea Twite |
Mamia ya mashabiki waliofurika kumpokea Twite |
Msafara wa mashabiki waliofurika kumpokea Twite kwenye Uwanja wa Ndege |
Biashara ya jezi inaendelea.... |
Hapa ni klabuni Jangwani.... mashabiki waliofurika kumkaribisha Twite nyumbani |
Karibu klabuni Twite... hapa ni Jangwani |
Katika mitaa ya Jangwani |
Katika mitaa ya Jangwani |
Katika mitaa ya Jangwani |
Halooo! Halooo... hunisikii vizuri? Usijali kuna kelele nyingi za shangwe za mahabiki wa Yanga hapa. Nakwambia hiviii..... Twite keshatua na wala hatumuoni huyo Rage akija na Interpol wala RB... |
Sijawahi kupokewa namna hii... Mbuyu Twite (katikati) akishukuru mashabiki kwa mapokezi makubwa waliyompa kutokea juu ya jengo la klabu ya Yanga |
Twite akipungia mashabiki kutokea juu ya jengo la Yanga baada ya kuwasili |
Asanteni sana... Twite akishukuru mashabiki waliojitokeza kwa mamia kwa ajili ya kumpokea. |
Yanga oyee... Twite akisalimia mashabiki Yanga |
HATIMAYE ile sinema ya beki Mbuyu Twite imefikia mwisho leo baada ya beki huyo mpya wa Yanga kutua jijini Dar es Salaam leo saa 9:15 alasiri akitokea jijini Kigali, Rwanda na kupokewa na maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo ya 'Wanajangwani'.
Beki huyo alilakiwa na mashabiki na kuvishwa jezi Na. 4 yenye jina la "RAGE', ambalo ni la mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage.
Awali, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Twite alipokewa na viongozi kadhaa wa Yanga wakiwamo Katibu Mkuu Selestine Mwesigwa na kigogo katika harakati za usajili, Seif Magari.
Beki huyo wa kimataifa wa Rwanda lakini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alibebwa juu juu na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wakimshangilia kwa miluzi, ngoma, matarumbeta na mavuvuzela.
Licha ya kuzuiwa na viongozi wake waliokuwa wakihofia vurugu za mashabiki ambao kila mmoja alikuwa akigombea kupata nafasi ya kumuona kwa karibu, Twite akafanikiwa kuzungumza kwa kifupi sana na kuelezea jinsi alivyoshangazwa na umati uliojitokeza kumpokea.
“Kwakweli siamini... nashukuru sana kwa kupewa heshima kama hii," akasema Twite.
"Nitacheza kwa nguvu na uwezo wangu wote ili kulipa fadhila hizi... kwakweli sikuwahi kufikiria kuwa kuna siku nitapokewa na watu wengi kiasi hiki. Sidhani kama nitasahau tukio hili,” aakasema Twite.
Kabla ya kuwasili kwa beki huyo wa zamani wa klabu za FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na APR ya Rwanda, kulikuwa na tishio kutoka kwa viongozi wa Simba, ambao walidai kwamba watahakikisha kuwa anatiwa pingu mara tu atakapokanyaga katika ardhi ya Tanzania.
Simba walichimba mkwara huo kutokana na tuhuma kwamba beki huyo kisiki amewalaghai kwa kusaini nao mkataba wa kuichezea timu yao na kisha kupokea dau la mamilioni ya fedha kutoka kwao, lakini mwishowe akawatosa na kukubali ofa ya mahasimu wao wa jadi, Yanga.
Hata hivyo, hakukuwa na polisi yeyote aliyeonekana kumkaribia Twite kwa nia ya kumkamata. Bali, askari waliokuwapo kwenye uwanja wa ndege wakati akiwasili walionekana kuwa 'bize' katika kuhakikisha kwamba hakuna uvunjifu wowote wa amani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope, amekaririwa akisema kuwa piga ua, ni lazima wamtie pingu Twite.
Akasema kuwa yeye yuko Mombasa nchini Kenya, lakini dhamira ya kumkamata Twite iko palepale na wenzake klabuni Simba watashirikiana kuhakikisha kwamba mchezaji huyo anafikishwa polisi.
No comments:
Post a Comment