Thursday, August 30, 2012
MAKUNDI YA LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA 2012-13... MAN UTD WANACHEEEKA, REAL MADRID KUNDI LA KIFO, ARSENAL SI MBAYA SANA, CHELSEA KUWAKABILI JUVE, INIESTA MWANASOKA BORA UEFA AWAPIKU MESSI, RONALDO
MONACO, Ufaransa
MABINGWA wa Ulaya Chelsea watakabiliana na mabingwa wa zamani Juventus, Shakhtar Donetsk ya Ukraine na timu inayoshiriki kwa mara ya kwanza kutoka Denmark, FC Nordsjaelland katikahatua ya makundi ya msimu huu kufuatia upangaji wa makundi uliofanyika leo.
Mfululizo wa mechi ngumu unatarajiwa katika Kundi D baada ya mabingwa mara tisa wa Ulaya, Real Madrid kupangwa dhidi ya mabingwa wa England, Manchester City, mabingwa wa Uholanzi, Ajax Amsterdam na mabingwa wa Ujerumani, Borussia Dortmund.
Bayern Munich, ambao walifungwa katika mechi ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa msimu uliopita na ambao walimaliza wa pili nyuma ya Dortmund katika Bundesliga, watawakabili Valencia, Lille na BATE Borisov wa Belarus katika Kundi F.
Barcelona, waliokuwa wakipewa nafasi kubwa msimu uliopita hadi walipotolewa na Chelsea katika nusu fainali, watawakabili mahasimu wao wa zamani Benfica, Spartak Moscow na Celtic.
Manchester United wamepangwa pamoja na Braga, Galatasaray na CFR Cluj katika Kundi H, wakati Arsenal watawakabili Schalke 04, Olympiakos Piraeus na Montpellier HSC ya Ufaransa aliyotokea mshambuliaji wao mpya Olivier Giroud.
Michuano hiyo itaanza Septemba 18-19 na fainali itafanyika kwenye Uwanja wa Wembley Mei 25.
Makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa ya Ulaya yaliyopangwa leo mjini Monaco:
Kundi A
Porto
Dynamo Kiev
Paris St Germain
Dinamo Zagreb
Kundi B
Arsenal
Schalke 04
Olympiakos Piraeus
Montpellier HSC
Kundi C
AC Milan
Zenit St Petersburg
Anderlecht
Malaga
Kundi D
Real Madrid
Manchester City
Ajax Amsterdam
Borussia Dortmund
Kundi E
Chelsea
Shakhtar Donetsk
Juventus
Nordsjaelland
Kundi F
Bayern Munich
Valencia
Lille
BATE Borisov
Kundi G
Barcelona
Benfica
Spartak Moscow
Celtic
Kundi H
Manchester United
Braga
Galatasaray
CFR Cluj
--------------------------------------------------------------------------------
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment