Wednesday, August 15, 2012

MBUNGE MPINA WA CCM LEO AMKABIDHI SPIKA VIELELEZO VINAVYOONYESHA MAJINA NA NAMNA VIONGOZI WA SERIKALI WALIVYOVUNA KIFISADI SH. TRILIONI 11 NA KWENDA KUZIFICHA KATIKA MABENKI YA USWISI...!

Mhe. Mpina... haki ya nani viongozi hawa ni mafisadi. Fedha zote hizi? Haiwezekani ...!

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
Hatimaye Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina amekabidhi ripoti kadhaa za mabenki ya Uswisi zinazoonyesha namna wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walivyojilimbikizia nchini humo fedha kufuru zinazofikia Sh. trilioni 11.

Kwa mujibu wa Mhe. Mpina, fedha hizo zilizotoroshewa Uswisi ni chafu na nyingi zimetokana na wizi na rushwa, hivyo akaitaka serikali ichukue hatua sahihi za kuchunguza na kutoa tamko lake.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vielelezo hivyo leo mchana, Mpina alisema kuwa amechukua hatua hiyo ili kukata mzizi wa fitna uliotokana na majibu yaliyokuwa yakitolewa na serikali bungeni kwamba hawana taarifa hizo.

Baada ya kumaliza muda wake wa kuchangia hoja ya Wizara ya Fedha, Mhe. Mpina aliyekuwa akishangiliwa sana na baadhi ya wabunge, alikwenda moja kwa moja katika meza ya Naibu Spika, Mhe. Job Ndugai na kukabidhi furushi la ripoti hizo.

Baada ya kuzipokea, Mhe. Ndugai aliahidi kuzikabidhi kwa serikali na pia akongeza kuwa kwa urahisi zaidi, ripoti hizo anazowasilisha Mhe. Mpina zinaweza pia kupatikana kupitia mtandao.

No comments:

Post a Comment