Daniel Sturridge |
Joe Hart |
LONDON, England
KIPA Joe Hart na straika Daniel
Sturridge hawatakuwamo katika kikosi cha timu ya taifa ya England
kitakachocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Italia keshokutwa
kutokana na majeraha.
Hart, kipa wa Manchester City ambaye
ni chaguo la kwanza katika timu ya taifa, hakuwamo pia katika kikosi cha klabu
yake kilichoshinda 3-2 dhidi ya Chelsea jana na kutwaa Ngao ya Jamii kutokana
na maumivu ya mgongo.
Hata hivyo, kocha wake Roberto Mancini
alisema kuwa tatizo alilo nalo "sio kubwa sana."
Straika wa Chelsea, Sturridge aliumia
kidole gumba cha mguu wakati alipoingia akitokea benchi kwenye uwanja wa Villa
Park.
Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy
Hodgson hajaita mchezaji mwingine yeyote kuziba nafasi za wawili hao, na hivyo
John Ruddy wa Norwich City atakuwa akipigania nafasi ya kuitwa kwa ajili ya
mechi hiyo itakayochezwa mjini Berne, pamoja na kipa Na.1 wa timu ya England
iliyoshiriki michezo ya Olimpiki, Jack Butland.
Andy Carroll, Jermain Defoe na Theo
Walcott ndio washambuliaji waliobaki kikosini. Mechi hiyo itakayochezwa kwenye
uwanja huru ni marudio ya robo fainali ya michuano ya Euro 2012 iliyoandaliwa
na nchi za Poland na Ukraine, ambapo kikosi cha kocha Cesare Prandelli kiliifunga
England kwa penati kabla na kutinga fainali.
No comments:
Post a Comment