Iker Casillas |
Cristiano Ronaldo |
Lionel Messi |
NAHODHA wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid, Iker Casillas amewaita Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuwa ndio wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa na akakiri kwamba sifa za kila mmoja uwanjani zinamfanya ashindwe kujua hadi sasa ni nani kati yao anayestahili kutwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia (FIFA
Ballon d'Or)
Kipa huyo ameendelea kukwepa kutoa msimamo wake juu ya nani atakayemchagua kati ya Messi na Ronaldo, ingawa alikiri kwamba kama uteuzi huo ungefanywa na yeye, basi angemchagua Ronaldo kwa sababu "ndiye anayemjua zaidi."
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Mexico, Univision, Casillas mesema: "Tunawazungumzia wachezaji wawili bora zaidi duniani kwa sasa na swali hili siku zote limekuwa likizua mjadala mkali. Baadhi wanadhani kwamba Messi ndiye bora zaidi, wengine wanaamini kwamba Ronado ndiye anayestahili. Siwezi kumchagua yeyote."
Pamoja na kusema hayo, nyota huyo wa Real Madrid alifichua hatimaye ni nani kati yao anayeweza kumpa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa Ballon d'Or.
"Kama nikitakiwa kuchagua mmoja wao, basi atakuwa Cristiano, ni kwa sababu ndiye ninayemjua zaidi kwani tunacheza pamoja katika ngazi ya klabu," amesema.
Casillas aliendelea kusema kwamba yeye anaamini kuwepo kwa wachezaji wawili bora zaidi duniani ni vizuri zaidi kuliko kuwa naye mmoja.
"Tunawazungumzia wachezaji wawili walio bora zaidi duniani kwa sasa, na ninafikiri kwamba kama angekuwa mmoja tu, isingekuwa vizuri sana kwa mchezo wa soka," alihitimisha kipa huyo mwenye miaka 31.
No comments:
Post a Comment