Prof. Mahalu (kushoto) akizungumza na Mwanasheria Alex Mgongolwa kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. |
Akitoa hukumu yake, Hakimu Mkazi Mfawidhi Illivin Mgeta amesema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kiasi cha kuwatia hatiani washtakiwa Mahalu na Grace.
Awali, hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa mwezi uliopita na Hakimu Katemana, kwa maelezo kuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mgeta aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo kukosekana kwavile alikuwa akikabiliwa na majukumu mengine.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na mawakili waandamizi wa serikali, Ponsiano Lukosi, Vincent Haule na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Linkolin, uliita mashahidi saba na vielelezo tisa vikiwemo mikataba miwili ya ununuzi wa jengo la ubalozi jijini Rome, Italia na upande wa utetezi uliita mashahidi watatu, akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa.
No comments:
Post a Comment