Kocha mpya wa Azam, Boris Bunjak "Boca" akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo asubuhi. |
AZAM FC leo imemtangaza kocha mpya raia wa Serbia, Boris Bunjak a.k.a Boca, ambaye amekuja kurithi mikoba ya Muingereza Stewart Hall ambaye amemaliza mkataba wake.
Boca ambaye amezaliwa mwaka 1954 na ana leseni ya ukocha ya UEFA, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Azam.
Mwenyekiti wa Azam, Said Mohammed, amesema Boca ambaye ana uzoefu wa kufundisha soka kwa miaka 22 katika klabu mbalimbali za soka za Serbia, Urusi, Ujerumani na Falme za Kiarabu pia aliwahi kuwa Mkufunzi katika Chama cha Soka cha Yugoslavia.
Mserbia huyo anaendeleza tabia mpya ya klabu za Tanzania kupenda makocha Waserbia tangu, Sredjovic Milutin 'Micho', Dusan Kondic, Kostadin Papic waliopita Yanga na Milovan Cirkovic wa Simba. WASIFU KAMILI BORIS BUNJAK 'BOCA'
Taarifa binafsi | |||
---|---|---|---|
Jina kamili | Boris Bunjak | ||
Tarehe ya kuzaliwa | Novemba 17, 1954 | ||
Taarifa za klabu | |||
Klabu yake ya mwisho | Al Oruba Sur | ||
Klabu aliyocheza* | |||
Miaka | Timu | Mechi† | (magoli)† |
FK Borac Cacak | |||
Timu alizofundisha | |||
1990-1993 | FK Sloga Kraljevo ) | ||
1995-1996 | FK Javor Ivanjica | ||
1996-1997 | Crvena Zvezda Gnjilane | ||
1999 | FK Radnicki Nis | ||
2000 | FC Uralan Elista | ||
2000-2002 | FK Mladi Radnik | ||
2002-2004 | FK Crvena Zvezda Beograd | ||
2004 | Al-Shaab | ||
2005 | FK Hajduk Kula | ||
2006-2007 | Al-Nasr | ||
2009- | Al Oruba Sur | ||
No comments:
Post a Comment