BARCELONA, Hispania
YOSSO Christian Tello hajapewa nafasi katika
kikosi cha kwanza cha Barcelona kilichotolewa leo ikiwa ni wiki chache tu kabla ya kuanza kwa msimu
mpya wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.
Straika huyo wa zamani wa klabu ya
Espanyol alichezeshwa sana katika kikosi cha Barca kuelekea mwishoni mwa msimu
uliopita, akishuka dimbani mara 22 katika michuano yote kuanzia Januari hadi Mei --
mwishoni mwa msimu wa 2011-12.
Licha ya kujumuishwa zaidi kikosini
msimu uliopita, yosso huyo bado hajapewa namba katika kikosi cha kwanza kinachojiandaa
kwa msimu mpya, na hayumo pia katika wasifu wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo uliomo
katika tovuti rasmi ya Barca.
Jordi Alba, mchezaji pekee hadi sasa aliyenunuliwa
na klabu hiyo katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, amepewa jezi Na.18,
sawa na aliyokuwa akiivaa wakati akiichezea timu ya taifa ya Hispania katika fainali
za Euro 2012.
Wote wawili, Alba na Tello
walikuwa sehemu ya kikosi cha kocha Luis Milla kilichoshiriki michezo ya
Olimpiki na kutolewa mapema katika hatua ya makundi kufuatia kipigo cha
kushangaza cha wiki iliyopita dhidi ya Honduras.
Barcelona watacheza mechi yao ya
kwanza ya La Liga Agosti 19 dhidi ya Real Sociedad.
No comments:
Post a Comment