Saturday, July 28, 2012

WENGER AGEUKA MBOGO KUULIZWA KUHUSU VAN PERSIE ARSENAL IKIPIGWA 2-0 NA MAN CITY

Arsene Wenger
Robin van Persie wa Arsenal akisikitika baada ya kukosa goli dhidi ya kipa Petr Cech wa Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Aprili 21, 2012.
Robin van Persie wa Arsenal akishuti mpira kuelekea langoni mwa Chelsea huku akichungwa na beki Gary Cahill wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Aprili 21, 2012.

Robin van Persie wa Arsenal akishangilia goli lao la tatu alilofunga dhidi ya Norwich City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London, England Mei 5, 2012.

ARSENE Wenger aligeuka mbogo jana baada ya kudai Arsenal haijapata ofa yoyote kwa ajili ya mshambuliaji Robin van Persie.


Licha ya Sir Alex Ferguson kusema kwamba Manchester United walituma ofa, Wenger alidai kwamba hawajapata ofa yoyote rasmi mezani kwa ajili ya nahodha wao anayetaka kuondoka.


Na kocha huyo wa Arsenal aliwaka baada ya timu yake kula kichapo cha 2-0 kutoka kwa Manchester City katika mechi yao ya kirafiki pale alipotakiwa kufafanua suala hilo.


"Tumeshazungumzia suala la Van Persie," alisema Wenger kwa sauti ya kuchukizwa. "Tunatoka kucheza mechi, kuna Waingereza wanne hapa lakini maswali yote manne yanamzungumzia yeye (Van Persie).


"Nimeshamzungumzia Van Persie na sitajibu swali lolote jingine kuhusu jambo hilo. Mmenielewa?"


Ingawa Arsenal walibainisha wiki iliyopita kwamba wamepokea kwa ajili ya Mholanzi huyo kutoka kwa United, City na Juventus, Wenger alijaribu kudai kinyume chake.


Mholanzi huyo hajaambatana na timu katika ziata ya ­Arsenal Mashariki ya Mbali, ili kuangalia uzima wake baada ya kucheza fainali za Euro 2012.


Wenger aliongeza: "Van Persie anakaribia kuwa fiti. Lakini hatujawasiliana tena na Man City United kuhusu yeye."


Roberto Mancini aliunga mkono madai ya Wenger kwamba hamna ofa iliyopelekwa kwa ajili ya Mholanzi huyo.


"Kama amesema hivyo, nadhani ni kweli. Van Persie ni mmoja wa washambuliaji bora hivyo ni vigumu kumnunua," alisema kocha huyo wa Man City.


Pablo ­Zabaleta na Yaya Toure walifunga magoli ya kipindi cha kwanza yaliyoipa Man City ushindi wa 2-0 kwenye Uwanja wa Bird’s Nest mjini Beijing, China.

No comments:

Post a Comment