Baadhi ya wanafunzi jijini Dar wakiandamana kutaka serikali imalizane na walimu. |
Wacheki wanafunzi hawa jijini Dar walivyoanza harakati za kudai haki kungali mapemaa...! |
Hatukubali hadi kielwekeeee....! Wanafunzi wakiandamana jijini Dar baada ya mgomo wa walimu wao |
Watazame na hawa wakati wakiandanamana Dar .... wana usongo kwelikweli wa masomo! |
Tunataaaaka.... haki yeeetu! Baadhi ya wanafunzi wa shule za Kijichi na Bwawani jijini Dar walivyokuwa wakiandamna |
Baadhi ya wale walioonekana wakiandamana leo kuelekea katika ofisi mbalimbali za serikali zinazoshughulia elimu ni wanafunzi wa shule za msingi za Tegeta na Mtakuja.
Wakizungumza na waandishi, baadhi ya wanafunzi hao walisema kuwa wanafanya hivyo ili serikali iongeze kasi ya kushughulikia mgogoro uliopo na kuumaliza ili hatimaye walimu wasitishe mgomo na kurejea madarasani.
Hatua kama hiyo ilichukuliwa pia na wanafunzi wa shule za Dar es Salaam na mikoa mbalimbali jana ambapo mjini Tunduma, polisi walilazimika kutumia nguvu ili kutawanya wanafunzi.
Miongoni mwa wanafunzi walioandamana jana ni pamoja na wa shule za Mbezi, Mbagala, Umoja wa Mataifa, Muhimbili, Bwawani, Mtoni Kijichi na nyingine kadhaa.
Chama cha Walimu (CWT), kupitia rais wake Gratian Mukoba, kilitangaza maandamano yasiyokuwa na ukomo kuanzia jana ili kushinikiza serikali itekeleze madai yao ya kuongezewa mishahara kwa asilimia 100, posho kwa kati ya asilimia 50-55 na posho ya mazingira magumu kwa asilimia 30.
Hata hivyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, amesema leo kuwa madai hayo hayatekelezeki kwani yanamaanisha kuwa mwalimu mwenye cheti atapaswa kulipwa mshahara wa Sh. 878,000 kutoka Sh.244,000 za sasa.
Badala yake, Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa ofa ya kupandisha mishahara ya walimu kwa asilimia 14 na pia kuunda Bodi ya Maslahi na Mishahara itakayofanya kazi kwa ajili ya wafanyakazi wa kada zote serikalini; hatua ambazo walimu walizipinga na kutangaza mgomo utakaoshirikisha walimu wote nchini kuanzia jana.
No comments:
Post a Comment