Ambulance ya magurudumu matatu kama hii ndizo alizolalamikia Mbunge wa Nkenge. |
Mhe. Asumpta Mshama (kushoto) |
Mbunge jimbo la Nkenge, Mhe.
Asumpta Mshama, amelalamikia uwezo mdogo wa ‘ambulance’ za magurudumu matatu na
kuihoji serikali kuwa itawasaidiaje akina mama wajawazito ambao wanashindwa
kuwahishwa hospitalini kutokana na udhaifu wa vyombo hivyo katika kumudu barabara
za jimboni kwake.
Mhe. Asumpta alihoji umadhubuti
wa ambulance hizo kwenye barabara mbaya za jimboni kwake wakati wa kupitisha vifungu
vya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa
mwaka ujao wa fedha.
“Maeneo kama ya Nkenge na Minziro
bajaji hizi huwa hazifiki… sasa naomba nielezwe kuwa serikali itawasaidiaje
akina mama wajawazito wa maeneo kama hayo?” Alihoji Mhe. Asumpta.
Akijibu swali hilo, Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alisema kuwa uamuzi wa serikali
kusambaza ‘ambulance’ za magurudumu matatu ni kusaidia utoaji wa huduma za afya
hasa kwa akina mama wajawazito pindi wanapotakiwa kuwahishwa hospitali kwani
ambulance za magari zinauzwa kwa gharama kubwa sana, ambapo gharama za gari
moja ni sawa na kununua ambulance za bajaji 10.
“Tutafanya tathmini na kuona
namna ya kusaidia watu wa maeneo hayo ambayo ambulance hizi (za bajaji) huwa
hazifiki,” alisema Dk. Mwinyi.
No comments:
Post a Comment