![]() |
Muwe mdaka hivi...! Kipa Iker Casillas akijifua na Valdes (kulia) na Pepe Reina wa timu ya taifa ya Hispania. |
![]() |
Usafiri wa 'pipa' mtamu sana... hapa Valdes akiwa ndani ya ndege na wachezaji wenzake wa Hispania, Iniesta (kulia) na Sergio Busquet |
![]() |
Valdes akishikilia kombe walilotwaa la Euro 2012 |
MADRID, Hispania
Kipa wa
klabu ya Barcelona, Victor Valdes amesema kuwa, ikiwa Iker Casillas wa mahasimu
wao wa jadi, Real Madrid atatwaa tuzo ya FIFA ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia
(Fifa Ballon d'Or) itakuwa ni heshima kubwa kwa makipa.
Hasimu huyo
wa Casillas katika mechi zao za watani wa jadi maarufu kama ‘el clasico’,
aliweka kando upinzani wao wakati wote wawili walipokuwa wakiitumikia timu ya
taifa lao la Hispania iliyotwaa ubingwa wa Euro 2012.
Baada ya Casillas
ambaye ni nahodha kuiongoza vyema Hispania katika fainali za Euro zilizoandaliwa
na nchi za Poland na Ukraine, kipa huyo wa Real Madrid amekuwa akitajwa na
baadhi ya wataalam wa soka kuwa ndiye anayestahili kuwa mshindi wa tuzo ya Mwanasoka
Bora wa Mwaka wa Dunia, jambo ambalo Valdes anaamini kwamba ni sahihi kama
kweli litatokea.
“Itakuwa heshima
kubwa kuwa na kipa mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or,” tkipa huyo wa Barca
aliviambia vyombo vya habari vya Hispania. “Hata hivyo kuna wachezaji wengine
ambao pia wanaweza kushinda tuzo hii. (Andres) Iniesta namkubali sana na
nimefurahi sana kwa kutambuliwa na kupewa tuzo alizo nazo."
HISPANIA =
BARCELONA
Valdes aliendelea
kueleza kwamba mtindo wa kucheza wa Hispania ulifanana na Barcelona, na pia akatoa
kauli ya kumuunga mkono kocha mpya wa Barca, Tito Vilanova.
![]() |
Tito Vilanova |
“Chini ya Vilanova
hakutakuwa na mabadiliko makubwa. Ni wakati wa kuwa makini na kutambua kwamba
baada ya (Pep) Guardiola kuna hatua nyingine. Namuamini sana kwa sababu namjua vizuri
kocha Tito,” alisema.
NEYMAR
Mwishowe,
Valdes pia alimzungumzia straika yosso mwenye kipaji wa Brazil, Neymar, ambaye
siku za nyuma alikuwa akihusishwa na uhamisho wa kwenda klabu za Barcelona na Real
Madrid.
"Neymar
ana kipaji cha ajabu. Anafanya vitu ambavyo ni vigumu kuiga. Ni mchezaji ambaye
timu yoyote ile itamtaka tu,” alihitimisha Valdes.
No comments:
Post a Comment