Monday, July 30, 2012

UPINZANI WATAKA MAAFISA USALAMA WALIOTAJWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIKA NA UTEKAJI DK. ULIMBOKA WACHUNGUZWE

Ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwanahalisi lililowatuhumu baadhi ya maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kuwa walihusika na tukio la kumteka Dk. Steven Ulimboka    
Dk. Steven Ulimboka alivyokuwa akionekana baada ya kufikishwa hospitalini.
Kambi ya upinzani bungeni imeitaka serikali kuchunguza na kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya maafisa usalama wa taifa waliotajwa ndani ya gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita kuwa ndio waliohusika na unyama wa kumteka, kumtesa na kumtupa kwenye msitu wa Mabwepande jijini Dar es Salaam kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.


Msemaji wa kambi ya upinzani ameyasema hayo bungeni mchana huu wakati akisoma hotuba ya kambi yao kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Dk. Ulimboka aliyekuwa mstari wa mbele wakat wa mgomo wa madaktari, alitekwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya kabla ya kuokotwa kwenye msitu wa Mabwepande. Hivi sasa anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini.

Gazeti la Mwanahalisi liliwatuhumu na kuwataja kwa majina baadhi ya maafisa usalama katika idara ya usaklama ya taifa kuwa ndio waliohusika katika kumteka na kumpiga vibaya Dk. Ulimboka kabla ya kwenda kumtupa Mabwepande.

Hata hivyo, Idara ya Usalama wa Taifa ilitoa taarifa ya kukanusha kuhusika na unyama huo na kuwataka wananchi wapuuze tuhuma hizo walizoziita kuwa ni 'uzushi'.

No comments:

Post a Comment