*AWATETEA PIA MADAKTARI WALIOFUTIWA USAJILI
Ukurasa wa mbele wa moja ya nakala za gazeti la Mwanahalisi. |
Mbunge wa Iramba Mashariki, Mhe. Tundu Lissu |
Mbunge wa Jimbo
la Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu, ameonyesha kusikitishwa na uamuzi
uliotolewa leo na serikali wa kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la kila
wiki la Mwanahalisi.
Mheshimiwa
Lissu amezungumzia masikitiko yake hayo jioni hii kabla hajaanza kuchangia mjadala
kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa
mwaka ujao wa fedha.
Lissu alisema
kwamba kwa watu wote wanaojua maana ya uandishi wa habari za kiuchunguzi,
taarifa za kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi ni sawa na giza nene.
“Kwa
wanaofahamu 'Investigative Journalism (uandishi wa habari za uchunguzi),
kufungiwa kwa Mwanahalisi kwao ni giza...,” alisema Mhe. Lissu.
Hata hivyo,
kabla Mhe. Lissu hajaeleza zaidi juu ya namna alivyoguswa na uamuzi huo wa serikali,
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, alimkatisha na kumtaka ajielekeze katika
kuchangia hoja iliyoko mbele yao kwa wakati huo; raia ambayo Mhe. Lissu
aliifuata na kuanza kujadili juu ya suala la kutimuliwa kwa madaktari hali ya
huduma za afya nchini.
Leo, serikali
imetangaza kulifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwa kile
kilichoelezwa kuwa ni kitendo cha gazeti hilo kuendelea kuchapisha habari na
makala za uchochezi.
KUTIMULIWA KWA MADAKTARI
Katika
kuchangia kwake, Lissu alisema kwamba inasikitosha kuona kuwa hivi karibuni serikali
imewafutia usajili madaktari zaidi ya 300 huku ikijua wazi kwamba taifa lina upungufu
mkubwa wa watu hao.
Akasema kuwa
ni vyema serikali ikaangalia uwezekano wa kuboresha maslahi ya kada hiyo na si
kuwafukuza pale wanapodai haki zao na kuwafanya wengine waende kutumika katika
maeneo mengine wanakothaminiwa zaidi na kulipwa vizuri kama Botswana.
“Inakuwaje
tunatumia fedha nyingi kusomesha madaktari, halafu tunawaachia wakatumikie nchi
nyingine kama Botswana?” alihoji Mhe. Lissu.
Akieleza
zaidi, Mhe. Lissu akasema kuwa madaktari waliofukuzwa (baada ya kugoma) hawakutendewa
haki kwa vile hawakupewa nafasi ya kujitetea, na kwamba uamuzi huo pia ni kosa
kwa mujibu wa sheria.
“Huwezi kushughulikia
tatizo la uvunjifu wa sheria, kwa kuvunja sheria... uongo mara mbili
hautengenezi ukweli mmoja,” alisema.
No comments:
Post a Comment