![]() |
Ni balaa....! Baadhi ya magari yakisombwa na mfuriko hayo nchini Urusi leo. |
KRASNODAR,
Urusi
Takriban watu
87 wamekufa baada ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kusababisha mafuriko
kusini mwa Urusi katika eneo la Krasnodar, maafisa wamesema leo.
Mafuriko
hayo ambayo hayakuwa yametabiriwa na wataalam wa hali ya hewa, yaliibuka ghafla
usiku wa kuamkia leo kuwakuta watu wengi wakiwa katika hali ya kutojua la
kufanya.
Vikosi vya
uokoaji kutoka katika jijila Moscow vimepelekwa kwa ndege na helikopta katika
eneo hilo. Picha za luninga zimekuwa zikionyesha mamia ya watu wakigombania
kukwea kwenye mapaa ya nyumba kwa nia ya kujiokoa.
Mbali na
kuua makumi ya watu na kujeruhi, mafuriko hayo yenye nguvu za ajabu pia
yamekuwa yakisomba magari na kubomoa miundomboinu ya barabara na makazi ya watu
takriban 13,000.
"Hadi
sasa hakuna umeme na maduka yamefungwa. Maelfu ya watu wamepoteza kila kitu na
sasa wanahaha kuokoa maisha yao,” alisema mmoja wa mashuhuda."
No comments:
Post a Comment