*ADAIWA KUVUTIWA NA ‘MIHELA’ CHINA
![]() |
Si unaona upenyo ule....! Keita akipokea maelekezo ya mwisho kutoka kw Guardiola kabla ya kuingia uwanjani. |
![]() |
Keita (wa pili kushoto) akishangilia goli na wachezaji wenzake wa Barca, kutoka kushoto ni Messi David Villa, Maxwell Scherrer na Dani Alves. |
![]() |
Seydou Keita (kushoto) na Alexis Sanchez wa Barca wakishikilia Kombe la Mfalme baada ya kulitwaa kwa kuifunga Athletic Bilbao kwenye Uwanja wa Vicente Calderon mjini Madrid, Mei 25, 2012. |
Kiungo wa
kimataifa wa Mali, Seydou Keita anaondoka Barcelona baada ya kuichezea kwa
miaka minne na kutwaa nayo makombe 14.
"Seydou
Keita amesema kwamba hataendelea kuichezea klabu hii msimu ujao," Barca walisema
kupitia tovuti yao (www.fcbarcelona.com).
"Barcelona
inamshukuru Seydou Keita kwa mchango wake katika miaka michache iliyopita na
kumtakia mafanikio mema."
Keita, 32, alijiunga
na Barca akitokea Sevilla kwa wakati mmoja na kocha Pep Guardiola.
Alikuwa na
uhusiano wa karibu na Guardiola na kuondoka kwake kunahusishwa na uamuzi wa kocha
huyo kutoendelea kuifundisha Barca baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.
Guardiola alimtumia
zaidi Keita kama mtokea benchi na kiungo huyo aliisaidia Barca kutwaa mataji
matatu ya La Liga (Ligi Kuu ya Hispania), mataji mawili ya Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya na mtaji mawili ya Kombe la Mfalme.
Vyombo vya
habari vya Hispania viliripoti kwamba kiungo huyo alikuwa na kipengele katika
mkataba wake unaomalizika 2014, kinachomruhusu kuondoka bure ikiwa hataanzishwa
katika kikosi cha kwanza katika walau nusu ya mechi za msimu.
Keita amekuwa
akihusishwa na uhamisho wa kwenda katika klabu ya Dalian Aerbin inayoshiriki Chinese
Super League, Ligi Kuu ya China, ambako huko anatarajiwa kuingia mkataba mnono
na kuvuna mabilioni ya pesa kama walivyofanya nyota wengine kadhaa, wakiwemo akina
Didier Drogba, Nicolas Anelka na Yakubu Aygbeni.
No comments:
Post a Comment