Saturday, July 14, 2012

MWANZA, MORO FAINALI COPA KESHO

Wachezaji wa timu ya Mwanza wakishangilia kwenye basi lao tayari kwa kuondoka kwenye Uwanja wa Karume baada ya kuitoa Kinondoni na kutinga nusu fainali ya Copa Coca Cola Jumatano. Timu ya Mwanza iliitoa Temeke katika nusu fainali na sasa itacheza fainali dhidi ya Morogoro kesho. Picha: Sanula Athanas

Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayozikutanisha timu za Mwanza na Morogoro itachezwa kesho (Julai 15 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanza saa 9 kamili alasiri.

Mwanza ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Temeke mabao 3-1 wakati Morogoro iliiondoa Tanga kwenye nusu fainali kwa ushindi wa mabao 3-1. Mechi zote za nusu fainali zilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Temeke na Tanga itachezwa kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 5 asubuhi. Mashindano ya Copa Coca-Cola 2012 yalianza Juni 24 mwaka huu yakishirikisha mikoa 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment